Tuesday, July 30, 2013

SOMA MUHIMU SANA.............BIDHAA 48 HAZITAKIWI SOKONI TBS IMETHIBITISHA.




Shirika la Viwango (TBS) limetangaza orodha ya bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena.

Hatua hiyo ya TBS inatokana na watengenezaji wa bidhaa hizo ambazo awali zilithibitishwa na TBS na kuruhusiwa kutumia nembo yao hiyo ya ubora kumalizika na wahusika kushindwa kuwasiliana na shirika hilo kwa ajili ya uhakiki wa bidhaa zao hizo.

Ofisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.

Bidhaa ziliazoainisha katika tangazo hilo ni pamoja na 
majina ya watengenezaji /wasambazaji katika mabano ni pamoja na karatasi laini ‘tissue’ za Alawi Supplies ya Zanzibar, Milk Marie Biscut za Britania, Maji ya Great Zone, Mishipi na nyavu za kuvulia samaki za Imara Fishnet, maji ya Raha na fulana za Kibo Trade.


Bidhaa zingine ni matofali ya GM Gross, taulo za watoto za Hengan Sanitary, baadhi ya rangi za Chui, beteri za Dry Cell, magodoro ya Jumbo foam, sabuni za Mbasira Investment ya Shinyanga, mifuko ya plastiki ya Centaza na mafuta ya kupikia ya Sun Flower Seed (Sun Shine) na korosho zinazosambazwa na Frabho Enterprises.

Pia taulo za wanawake za Sythentic Detergent (ARIEAL) za Procter&Gambler, mifuko ya B-Twill Jute na A-Twill, mifuko ya plastiki ya Tropical, mafuta ya kupikia ya Sun Flower ya A TO Z Oil Mills, Korosho za Munawar ya Mbeya, Sabuni za kunawia za Brite Chemicals, pipi, lawalawa, mipira ya kutafuna ya rangi mbili.

Vilainisha vya injini (Saud Oil) za Star Composed, betri za 777 kutoka China, maji ya kunywa ya Shia yanayotengenezwa na Siha Beverage, mtindi wa Morani Dairy ya Tanga, pikipiki za Star Shineray, vigae vya Mbezi, sabuni ya Liquid Detergent, mbao zilizotiwa dawa za Mombo, Jam iliyochanganywa ya Les Group ya Musoma.

Orodha hiyo pia inataja Jusi za nanasi za Unnat Fountain ya Morogoro, Maji Uluguru, springi za magari za kampuni ya TASIA, Gypsum zinazotengenezwa na Tanzania Gypsum ya Dar es Salaam, Maji ya Uzima, magodoro ya Plyfoam,Mvinyo wa nanasi wa Kivumbui ya Arusha na mabati ya RD Roofing & Wire Product.

Bidhaa zingine ni unga wa sembe wa Kweniml ya Machame Kilimanjaro, boriti za Ravji Manufacturing, mafuta ya breki za magari ya Automotive Packed ya Dar es Salaam, maJi ya kunywa ya AAMFA, pikipiki za Foshan Fost za China na mvinyo wa matunda wa Victoria Food Product ya Mara pia Jibini, mtindi na maziwa ya Kyaka Milk Processing , Sabuni za kufulia za Jamii za Kampuni ya Mbasira ya Shinyanga.

SIKILIZA NA DOWNLOAD:.. WISE ONE ft JACO BEATS - MALAIKA (PEREMENDE MUSIC EMPIRE)

Produced by JACO BEATS, PEREMENDEE MUSIC EMPIRE BADO WANAENDELEZA UBABE KANDA YA KATI NA HII NI NGOMA YAO MPYA.


BOFYA  HAPA KUDOWNLOAD

PEREMENDE MUSIC EMPIRE DROPS NEW VIDEO:.....WISE ONE ft JACCO BEATS - MALAIKA (OFFICIAL VIDEO)


WATCH AND DOWNLOAD IT HERE

SIKILIZA NA DOWNLOAD SNURA - NIMEVURUGWA




BOFYA HAPA KUDOWNLOAD

DOWNLOAD NEW MUSIC.... JOH MAKIN ft NIKKI wa PILI - BEI YA MKAA.


ILI KUDOWNLOAD BOFYA  hapa

WHY ALWAYS CLOUDS FM!!!!!!!!...."SINA MPANGO WA KUAJIRIWA NA "K....MA" YOYOTE.... (MWISHO MWAMPAMBA)



HALI SI SHWARI KATI YA KITUO CHA MATANGAZO CHA CLOUDS FM NA MWISHO MWAMPAMBA.........

 Mwisho Mwampamba amegeuka  mbogo  na  kufurumua  matusi  ya  nguoni  kwa  Clous Fm  baada  ya  kituo  hicho  kuanza  kumjadili  na  kumchambua...

Mwampamba, ambaye  ni  staa  namba  mbili  wa  shindano  la  big  brother  mwaka  2003  anadai  kutoridhishwa  na  kitendo  cha  Cloud  fm kuanza  kumjadili...

Staa  huyo  amedai  kwamba  yeye  anamaisha  yake  na  hivyo  haoni  haya  ya  kuanza  kufuatiliwa  kwa  kuwa  hana  mpango  wa  kuomba  ajira  kwa  yeyote...

"Clouds fm siwaelewi mnatafuta nini . Nahisi mnatafuta kupakazwa mafuta ya ubuyu . Tafadhali kusaga naona heshima inapungua . 


"Had mifugo yako hujawalea vizuri . Mimi sio msanii na pia sita ajiriwa na k**ma wowote yule . Stay away from me n my family.Ameandika  staa  huyo  katika    account  yake  ya  facebook


SIKILIZA NA DOWNLOAD NGOMA HII:...... A-TOWN HAITAWALIKI- KAPUKU DIGITAL

Ukipata nafasi ya kusikiliza nyimbo hii utagundua kitu kutoka arusha ndani yake yameongelewa mengi sikiliza mwenyewe............




BOFYA HAPA KUDOWNLOAD

MAJINA YA WAUZA UNGA (madawa ya kulevya) HADHARANI : IMEANDIKWA NA WAFUNGWA HONG KONG WENYE ASILI YA KITANZANIA.


CLICK PAGE UNAYO ITAKA KUVIEW VIZURI








SOURCE HAPA

Monday, July 29, 2013

TEAM TRUTH TUNAOMBA RADHI KWA POSTI ILIYOPITA "KUHUSU KUAPDATE ACCAUNT YA MIKOPO'

Tunaomba radhi kwa posti ya kuapdate mikopo iliyo tolewa leo...................... upotoshaji huo umefanywa na moja ya team member wetu baada kusikia habari hizo tangu asubuhi kama ADMIN wa team truth naomba radhi na nachukua nafasi hii kusema kwa wanotakiwa kuapdate na wale tu ambao hawakupata nafasi tya kuupdate mwanzo account zao mwanzo................... POSTI HIYO KWA SASA HAIPO.

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA NA KEEP IN TOUCH

DOWNLOAD NA SIKILIZA NGOMA MPYA YOUNG DEE - KIJUKUU


INGIA HAPA KUDOWNLOAD

TANGAZO KWA UMMA: HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOAN BOARD


TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawatangazia waombaji wote wa mikopo wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo kuwa mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ni tarehe 31 Julai, 2013 na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawasisitizia waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: www.olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti:www.heslb.go.tz kabla ya tarehe 31 Julai, 2013.
Kila mwombaji anakumbushwa kusoma kwa umakini mwongozo wa ujazaji wa fomu ya maombi ya mikopo kwa mwaka 2013/2014 na kulipia ada ya shilingi 30,000/= kwa waombaji wapya kwa njia ya M-Pesa.

Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

SIKILIZA NA DOWNLOAD JACO BEATS - KILAZA (PEREMENDE MUSIC EMPIRE)


BOFYA HAPA KUDOWNLOAD

Sunday, July 28, 2013

SIKILIZA NA DOWNLOAD NEW HIT "VAN B ft TCHAZ - LAWAMA"



BOFYA HAPA KUDOWNLOAD.

PEREMENDE MUSIC EMPIRE IMEPOKEA VIFAA VIPYA "KEEP IN TOUCH"


Recording label "peremende Music Empire" yenye maskani yake mjini Dodoma imepokea vifaa vipya vya production kutoka UK, akiongea na TEAM TRUTH  the CEO Erick Backamaza amethibitisha hilo na kuwataka watanzania kujiaanda kwa project tu.
................." sa ivi ni mawe baada ya mawe nimepokea vifaa vipya kutoka mbele na sasa tupo katika project ya kutengeneza muvie inayoitwa "40 DAYS" hivyo watanzania kaeni mkao"............ amen ma men.......
kwa sasa peremende ndo label inayo fanya vizuri zaidi kutokea Dodoma... kila la heri katika mafanikio yenu.

LULU: "SIKU HIZI NASALI NA NAMUAMINI MUNGU NATAMANI NINGEISHI HIVI NYUMA".





MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. 


Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza

KAULI NZITO: TEAM TRUTH LIVE KATIKA KONGAMANO LA MUSTAKABALI WA AMANI NA USALAMA WA TAIFA LETU KWA MIAKA 50 IJAYO UDSM.




 HAYA NI BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA KATIKA KONGAMANO HILO KATIKA RED NA MAJINA YA WACHANGIAJI (team truth inaomba radhi endapo majina haya yamekosewa) 

Chama kilichoko madarakani kisiwe chama dola ili kuleta usawa…………… PROF. Mpangala Gaudence. 

Tutauawa sana… Tutafungwa sana… Tutaonewa sana kwa sababu mfumo unaoendesha nchi umeparaganyika……………. MH. Tundu lisssu

Liliani Wasira………….. ( mwanasheria) tusitafute mchawi tunamjua na ni serikali kulewa madaraka na watanzania kuwa waoga. wanaume lazima mthubutu msiwe waoga MH. PINDA karahisisha kwamba serikali imechoka na fimbo ya mnyonge ni kura.

IDDI MAJUTO,……………. wanasiasa wa tanzania wanajuana na lao ni moja na ndo mana wancheza mziki pamoja hivyoikitokea vita mtanzania wa kawaida ndie atake umia

MIGOMO ELIMU YA JUU……….. FAHAMI… vyombo vya habari vinapotosha ukweli kuhusu migomo elimu ya juu.. waziri mkuu katupilia mbali mapendekezo 16 kuhusu migomo. viongozi kukaa kimya hasa muheshimiwa raisi ni uoga wakuwakabili wasomi.

MAYROSE… (MWANAHARAKaTi WA MAENDELEO)… kiongozi ni taa nimtu wa kuonesha njia …waziri mkuu mtoto wa mkulima amekidharau kilimo kwamba ni duni,

 Dr. SLAA. mchawi wetu hayuko nje ni serikali huku akionesha waraka mballimbali ikiwemo tume mbalambali zilizoundwa, tume ya haki za binadamu imetoa taarifa ya mauaji na serikali imeificha, jeshi linapoteza hadhi (huku akiomba radhi) serikali nitatizo la ardhi, elimu ni duni tatizo ni serikali

MWAKILISHI NCCR MAGEUZI…. nguvu ya hoja ndo siasa ya nccr na si kulalamika.

PILLI SAIDI (MWANAHARAKATI)… maandamano ni haki ya kikatiba.. baadhi ya yama vya siasa hutumia maandamano na vijana kutekeleza matakwa yao hivyo serikali iwe na njia mbadala ya vijana kujiajiri kuepusha maandamano yasiyo lazma. vyombo vya habari vitumie busara katika kulinda amani ya nchi kwani wanaoumia ni sisi.

AMAN MUHONJWA (MUHITIMU UDSM)……… tanzania haina amani bali utulivu tu huku akitaja matukio baadhi ikiwe lile la mabomu, miaka 50 ijayo ni giza huenda wajukuu zetu hawatoiona amani kabisa

BW. JUSTIN………..watanzania tufikiri tuko wap, utele na kufikika vinahitaji uongozi bora. polisi wanafanya kazi nzuri na wanaweka uzazi wa mpango na kosa la jinai halifichiki ipo siku utakuja na utahukumiwa

JENERALI….. hakuna vitendo vya ubakaji mtwara hizo ni propaganda zinazo katisha tamaa na si kila mwana siasa angependa kuiona hali ile mtwara (amani) NAIBU KATIBU MKUU CUF…… hali ya amani inavunjwa na vyombo vya dola vithibitisho vya ubakaji mtwara vipo na kamshangaa jenerali kukanusha.

KATIKA HILI NAPE NAUYE UNAKOSEA: "WALIOPENDEKEZA SERIKALI TATU NI WAZEE WANAOSUBIRI KUFA"

MZIMU wa serikali tatu bado unaendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo jana, Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipinga tena uwepo wa serikali tatu na kudai kuwa waliotoa maoni hayo ni wazee wanaosubiri kufa. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili mchakato wa Katiba Mpya, katika ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye alisema nia ya serikali tatu ni kuleta matabaka ambayo yatasababisha migogoro. “Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja Muungano enzi za ujana wao? Wamenufaika na Muungano kwa kipindi cha miaka 50, sisi vijana wanataka kutuachia mgogoro!”alisema Nnauye. Nape alisema kuvunjwa kwa Muungano kutasababisha mgogoro mkubwa wa rasimu kutokana na muda ambao Muungano huo umedumu. Alisema kuundwa kwa serikali tatu si sera ya CCM kama wanavyodai wapinzani, bali ni maoni ya watu waliyoyawasilisha katika ukusanywaji wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya. “Sera ya CCM ni kuongoza serikali mbili na si tatu, na hii sera tutaendelea kuitetea na kuilinda mpaka mwisho wa dunia, tunachoamini katika chama chetu hatuogopi kutetea sera ambazo tumezitoa wenyewe,” alisema Nnauye. Alisema ni vyema zikamalizwa kasoro zilipo katika mfumo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na si kuongeza madaraka yasiyo na tija. Nape alisema kitendo cha Tume ya Jaji Joseph Warioba kusema imetumia sheria ya mwaka 1964 kuwa kigezo cha kuundwa kwa serikali tatu si sahihi, kutokana na makubaliano ya mwaka huo kwamba ni serikali mbili. Kiongozi huyo wa CCM pia alishangazwa na kitendo cha Rasimu ya Katiba mpya kutamka wazi idadi ya mikoa pamoja na wilaya ambazo zitatumika katika uchaguzi na kwamba mwenye jukumu hilo ni Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. “Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa serikali tatu itaelea katika madaraka, kwani serikali ya Tanganyika itakuwa haiwezi kuwatetea wananchi, hali itakayosababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa urasimu ambao ni adui wa maendeleo,” alisema Nnauye. Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa Muungano kutasababisha kuiburuza Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani asilimia 95 ya uchumi wa visiwani unategemea Tanzania Bara. Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa kiongozi ni kuwatetea wananchi na si kuwazidishia mizigo. Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Nnauye alisema CCM hakiogopi mgombea binafsi, kwani hata akigombea chama hakitapata hasara yoyote. Nape alisema sera ya CCM ni kukataa wagombea binafsi wanaouza unga na si kukataa mgombea binafsi kama ambavyo vyama vingine vya siasa vinavyodai katika vyombo vya habari. Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9 inazungumzia umri wa Mbunge kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa CCM suala hilo si sahihi, kwani wabunge wenye miaka 21 wanawajibika vizuri kuliko wazee. Mtanzania

SIKILIZA NA DOWNLOAD CentalZone - Tukutane bank



BOFYA  HAPA KUDOWNLOAD