Sunday, July 28, 2013

KAULI NZITO: TEAM TRUTH LIVE KATIKA KONGAMANO LA MUSTAKABALI WA AMANI NA USALAMA WA TAIFA LETU KWA MIAKA 50 IJAYO UDSM.




 HAYA NI BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA KATIKA KONGAMANO HILO KATIKA RED NA MAJINA YA WACHANGIAJI (team truth inaomba radhi endapo majina haya yamekosewa) 

Chama kilichoko madarakani kisiwe chama dola ili kuleta usawa…………… PROF. Mpangala Gaudence. 

Tutauawa sana… Tutafungwa sana… Tutaonewa sana kwa sababu mfumo unaoendesha nchi umeparaganyika……………. MH. Tundu lisssu

Liliani Wasira………….. ( mwanasheria) tusitafute mchawi tunamjua na ni serikali kulewa madaraka na watanzania kuwa waoga. wanaume lazima mthubutu msiwe waoga MH. PINDA karahisisha kwamba serikali imechoka na fimbo ya mnyonge ni kura.

IDDI MAJUTO,……………. wanasiasa wa tanzania wanajuana na lao ni moja na ndo mana wancheza mziki pamoja hivyoikitokea vita mtanzania wa kawaida ndie atake umia

MIGOMO ELIMU YA JUU……….. FAHAMI… vyombo vya habari vinapotosha ukweli kuhusu migomo elimu ya juu.. waziri mkuu katupilia mbali mapendekezo 16 kuhusu migomo. viongozi kukaa kimya hasa muheshimiwa raisi ni uoga wakuwakabili wasomi.

MAYROSE… (MWANAHARAKaTi WA MAENDELEO)… kiongozi ni taa nimtu wa kuonesha njia …waziri mkuu mtoto wa mkulima amekidharau kilimo kwamba ni duni,

 Dr. SLAA. mchawi wetu hayuko nje ni serikali huku akionesha waraka mballimbali ikiwemo tume mbalambali zilizoundwa, tume ya haki za binadamu imetoa taarifa ya mauaji na serikali imeificha, jeshi linapoteza hadhi (huku akiomba radhi) serikali nitatizo la ardhi, elimu ni duni tatizo ni serikali

MWAKILISHI NCCR MAGEUZI…. nguvu ya hoja ndo siasa ya nccr na si kulalamika.

PILLI SAIDI (MWANAHARAKATI)… maandamano ni haki ya kikatiba.. baadhi ya yama vya siasa hutumia maandamano na vijana kutekeleza matakwa yao hivyo serikali iwe na njia mbadala ya vijana kujiajiri kuepusha maandamano yasiyo lazma. vyombo vya habari vitumie busara katika kulinda amani ya nchi kwani wanaoumia ni sisi.

AMAN MUHONJWA (MUHITIMU UDSM)……… tanzania haina amani bali utulivu tu huku akitaja matukio baadhi ikiwe lile la mabomu, miaka 50 ijayo ni giza huenda wajukuu zetu hawatoiona amani kabisa

BW. JUSTIN………..watanzania tufikiri tuko wap, utele na kufikika vinahitaji uongozi bora. polisi wanafanya kazi nzuri na wanaweka uzazi wa mpango na kosa la jinai halifichiki ipo siku utakuja na utahukumiwa

JENERALI….. hakuna vitendo vya ubakaji mtwara hizo ni propaganda zinazo katisha tamaa na si kila mwana siasa angependa kuiona hali ile mtwara (amani) NAIBU KATIBU MKUU CUF…… hali ya amani inavunjwa na vyombo vya dola vithibitisho vya ubakaji mtwara vipo na kamshangaa jenerali kukanusha.

No comments:

Post a Comment