Saturday, July 27, 2013

DOWNLOAD NA SIKILIZA NYIMBO YA CLIMAX - UJUZI

BONYEZA HAPA:
http://www.hulkshare.com/w9mm55kl3sw0

MISRI HALI SI SHWARI INASEMEKANA NI HALI MBAYA ZAIDI KUWAHI KUTOKEA TANGU RAISI ANG'OLEWE MADARAKANI.

Daktari katika hospitali ya muda amesema watu wawili walifikishwa wakiwa kichwa na viwili wili vyao vimetenganishwa huku wengine wakiwa na matundu ya risasi vichwani na kifuani.Muslim Brotherhood wamelilaumu jeshi kwa kuwapiga risasi na kuwauwa wafuasi wao.Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi wamesema zaidi ya watu laki moja na ishirini wameuwawa katika mapambano na vikosi vya ulinzi na usalama mjini Cairo.

Polisi waliingia katika mkusanyiko wa usiku wa wafuasi wa Morsi saa chache baada ya waziri wa mambo ya ndani kusema wafausi wa Morsi na chama chao cha Muslim Brotherhood waliokusanyika kwenye viunga vya msikitini wa Rabba Al Adawiya lazima waondoke.
Hospitali hiyo imekuwa katika hali ngumu ya kumudu miili ya marehemu na majeruhi wanaofikishwa hospitalini hapo.
Mwandishi wa BBC anasema ni mapigano mabaya zaidi tangu jeshi limuondoe rais Morsi madarakani.
Wakati huo huo, Uingereza imekemea matumizi ya nguvu yanayopoteza maisha ya watu nchini Misri.
Waziri wa masuala ya kigeni William Hague amewataka wenye mamlaka kumaliza mapigano na vurugu hizo.
Amesema wale waliohusika na mauaji hayo ni lazima wawajibike na haki ya wanaoandamana kwa amani ni wajibu ilindwe.
Bwana Hague pia amelitaka jeshi kuwachilia huru viongozi wa Muslim Brotherhood waliowekwa kizuizini akiwemo rais Mohamed Morsi.
via BBC SWAHILI

Friday, July 26, 2013

KWA UFAHAMU ZAIDI KUHUSU SHERIA ZA KAZI TEMBELEA LINK HII NA DOWNLOAD (attachment).


http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/24624-tanzania-labour-law-sheria-ya-kazi-tanzania.html

KIKWETE: IGUSE TANZANIA UKIONE CHA MOTO.... WATANZANIA LALENI KWA AMANI.


RAISI JAKAYA KIKWETE ametuma ujumbe kwa wale wanaoitisha tanzania. amewaambia wakithubutu watakiona cha mtema kuni kama ilvyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda
Alisema mamlaka za ulinzina usalama zilimdhibitiAmin alipofanya uvamizi katik ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingineyeyote atakaechezea usalama wa nchi. 

Wakati raisi akiyasema hayo, Mkuu Wa Majesh, Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wowote jeshi lipo imara na kuwataka wasiogope lolote.
Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya iliyopo Muleba, Kagera.
“Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wakati wowote, saa yoyote tuko tayari kulinda nchi yetu. Hatuko tayari kuona amani inaharibika nchini, hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kuimega au kuichezea nchi yetu kama alivyofanya Idd Amin.”Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanzania.
Jenerali Mwamunyange alisema jeshi wakati wote liko imara kuwalinda wananchi na nchi kwa jumla hivyo wasiogope...“Endeleeni na shughuli zenu na msiogope mtu yeyote, fanyeni kazi zenu bila wasiwasi.” Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo, Jenerali Mwamnyanye alisema yeyote atakayethubutu kuchezea usalama wa nchi atakiona cha mtema kuni. Akizungumzia Siku ya Mashujaa, Rais Kikwete alisema ni siku ya kuwakumbuka mashujaa waliojitolea maisha yao wakati wa Vita ya Kagera kuilinda nchi yao ili iwe salama na yenye amani. 
“Kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama yake kwani kuna wengine walikufa na wengine wakabaki na vilema kwa ajili ya hilo. Wale ambao wamebaki na wana matatizo lazima tuwaangalie vizuri na vile ambavyo havijafanyika tutavishughulikia kwani kutetea taifa ni kazi ngumu.”
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu ambao wote walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Awali, viongozi wa dini, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini, Shehe wa Mkoa, Haruna Kichwabuta na Mwakilishi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo, Askofu Elisa Buberwa walitoa wito kwa Watanzania kuthamini amani iliyopo na umuhimu wa kuwa na mshikamano katika kuilinda na kuhakikisha kwamba haivurugwi kwa misingi ya imani, itikadi au ukabila.
Matatizo Muleba
Awali, Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi wa Muleba kuwa matatizo ambayo wabunge wao wameyawasilisha kwake mbele yao atayashughulikia.
“Nimesikia yale waliyoyasema hapa ; suala la mpaka kati ya eneo la wananchi na jeshi, Waziri wa Ardhi yupo hapa, kaeni na jeshi na vijiji ili tatizo liishe ni jambo ambalo linawezekana hivyo litatuliwe,” alisema Rais Kikwete.
Alisema suala la umeme na madaraja litashughulikiwa na viongozi wa mkoa wakishirikiana na wabunge na watakapokwama wafikishe kwake... “Mimi ndiye ninayetoa fedha za maendeleo hivyo hayo masuala yakikwama waniambie nitayashughulikia.” Chanzo: Mwananch

HURUMA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER: HII NDIO HALI YAKE BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI.

MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

 Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

 Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki. Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua. Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni. Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake