Monday, August 12, 2013

AJALI AJALI AJALI AJALI........... MPAKA LINI?



Lilikuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Arusha, lilipata ajali maeneo ya barabara ya Chalinze- Segera Bagamoyo. Abiria wawili wamefariki dunia na wengine 63 wamejeruhiwa na kulazwa katika vituo vya afya kadhaa, zahanati pamoja na Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani baada ya basi mali ya Kampuni ya Meridian kuacha njia na kupinduka jana katika Barabara Kuu ya Chalinze- Segera wilayani Bagamoyo mkoani Pwani

Abiria waliofariki ni miongoni mwa majeruhi 24 wa ajali hiyo ambao walipelekwa moja kwa moja kupata matibabu katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi baada ya hali zao kuonekana ni mbaya zaidi ya wengine katika eneo la tukio. Wengi walikuwa wamevunjika sehemu mbalimbali za miili yao.
Kamanda wa Polisi Pwani Ulrich Matei alithibitisha kutokea ajali hiyo.

Akizungumza hospitali hapo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya hiyo, Dk Peter Dattan alithibitisha kupokea baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya 24 waliofikishwa hapo wawili walifariki na wote ni wanaume majina yao bado hayajajulikana.
Dk Dattan alisema majeruhi 22 wanaendelea kupatiwa matibabu na kati yao wanawake ni 12 na kwamba kwa jumla hali zao wote ni mbaya kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata.
Naye Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Chalinze walikolazwa majeruhi wengine Dk ,Victor Bamba akizungumza kituoni hapo alisema majeruhi waliofikishwa hapo ni 12.

Alisema majeruhi watatu kati ya hao walikuwa wakifanyiwa mpango wa kupelekwa Tumbi baada ya hali zao kubadilika na kwamba wengi wao wameumia zaidi sehemu za kichwani, kuvunjika miguu, mikono na mbavu
Dk Bamba aliiomba Serikali na wadau wa afya kuhakikisha kuwa utoaji na usambazaji dawa na vifaa tiba unalenga kwenye maeneo yenye ajali nyingi za barabarani ili kuweza kupatikana dawa na vifaa tiba kwa wakati pindi inapotokea matukio ya ajali.
Kwa mujibu wa mashuhuda na wakazi wa Kijiji cha Kimange, Hamis Shaaban na Yusufu Mzee walisema ajali hiyo ilitokea saa 5.40 asubuhi jana
mwananchi.

UTAMJUAJE MWENYE MAPENZI YA KWELI?????



Nimeandika mada hii kutokana na watu wengi kushindwa kutofautisha kupendwa kweli na kutamaniwa. Wapo walioingia mkenge kwa neno hilo hasa walio wageni katika uwanja huu wa mahaba. Ukiambiwa unapendwa basi unachanganyikiwa na kusahau maneno matupu hayajengi nyumba.

Nina maana gani?

Watu wengi wamekuwa wakitumia neno hili kama mtego wa kumpata mtu, kwa kujifanya anakupenda sana na nahau nyingi za mapenzi ambazo zinaweza kukufanya masikio yako yazibe na kuona nani kama wewe.

Siku zote mtafutaji ana lugha tamu ya mapenzi na kabla ya kutamka lolote lazima atangulize nakupenda sana na kuongezea ajuavyo. Hii si mara moja watu kuingia mkenge inapotokea wanakutana na hali hiyo.

Lazima uelewe serikali ya mwili wako inakutegemea wewe, ukiipeleka vibaya lawama zitakuwa juu yako. Usiwe na papara ya kutoa uamuzi wa kukubali uambiwavyo unapendwa bila kufikiria kwa kina. Hakuna hata siku moja mtu anayekutaka kimapenzi akuambie anakuchukia.

Fikiri kabla ya kutenda na kuona kauli uliyopewa ina nia gani na wewe, kweli anakupenda au anataka kukuchezea na kukuacha.

Katika uchunguzi wangu nimegundua wengi hupima kwa masikio juu ya kile aambiwacho na si kufikiria nini hasa kilichomvutia aliyekutamkia maneno hayo. Japo kakutamkia anakupenda, ni vema ukafanya kadiri uwezavyo kupata muda kufikiria kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wowote ambao unaweza kukufanya uwe na faida au hasara.

Neno nakupenda siyo mapenzi kamili, bali tabia ya mtu na kuonyesha kweli anakupenda kwa dhati. Akupendaye huwa hana haraka ya kufanya ngono, hufuata taratibu zote ili mradi kujenga uaminifu moyoni mwako.

Hii hutokana na kuwa na uhakika wewe ni wake, hana hofu ya kutanguliza ngono mbele katika uhusiano wenu wa kimapenzi. Ukiona umekutana na mtu anayetanguliza ngono baada ya neno nakupenda huyo hakupendi bali anakutamani.

Tumekuwa tunatumia neno nakupenda kama kiwakilishi cha ujumbe wa mapenzi na si penzi kamili.
Mapenzi ya kweli ni ya vitendo na si maneno, anayekupenda utamjua tu wala hajifichi. Atakuwa mpole, mwenye huruma, anayekujali, muaminifu na mtu aliye muwazi mwenye kukupa uhuru wa kumjua kwa undani ili kukuondoa wasiwasi.

Mapenzi mengi ya siku hizi yamekuwa ya usiri mkubwa yenye mipaka. Kama kweli anakupenda kwa nini akudanganye na akuwekee mipaka ya kumjua? Wakati huo mdomoni kwake ana kila nahau tamu za kimapenzi na kulitamka neno nakupenda kama kiwakilishi.

Huyo si mkweli wala hana mapenzi bali ni muongo aliyejificha nyuma ya neno nakupenda. Kuwa macho na watu hawa sipendi kesho uniulize swali hili.source ya mada hii,Muandishi Joseph shaluwa

HOTUBA YA MUGABE BAADA YA UCHAGUZI


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anatarajiwa kutoa hotuba yake ya kwanza tangu kushinda uchaguzi mkuu wa Zimbabwe zaidi ya wiki moja iliyopita. Mugabe atahutubia umma wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya mashujaa mjini Harare kuwakumbuka wale waliofariki wakipigania uhuru wa taifa hilo.
Chama pinzani cha MDC, chake waziri mkuu Morgan Tsvangirai, kitasusia sherehe hizo.

Chama hicho kimewasilisha malalamiko yake kuhusu uchaguzi mkuu ambao kinasema ulikumbwa na wizi wa kura kikitaka uchaguzi huo kurejelewa.Bwana Mugabe alishinda 61% ya kura kwenye uchaguzi huo uliokamilika tarehe 31 mwezi Julai, huku mpinzani wake Morgan Tsvangirai akichukua nafasi ya pili kwa 35% ya kura zilizopigwa.

Chama cha Mugabe Zanu-PF kilishinda wingi wa viti vya bunge kikipata zaidi ya thuluthi mbili ikiwa ni viti 160 ya viti kati ya 210 vya bunge zima.Sherehe za kuadhimisha siku ya mashujaa Zimbabwe, ni sherehe za kujivunia kwa wazimbabwe wakati ambapo nchi hiyo ilijipatia uhuru wake miaka ya sabini.
Hii leo Mugabe atatoa hotuba yake ya kwanza katika eneo la kumbukumbu la vita hivyo na ambako baadhi ya wapigania uhuru wamezikwa.
Hotuba za Mugabe zinasifika zaidi kwa siasa zake kali za kizalendo, na ambazo zaidi hulenga mkoloni wake wa zamani Uingereza na pia anatarajiwa kujipiga kifua kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi mkuu uliopita mwezi jana.

Chama cha MDC kinasusia sherehe hizo katika kile kinachosema ilikuwa wizi mkubwa wa kura uliofanywa na chama cha Zanu-PF, kwa hivyo sherehe hii bila shaka itazongwa na siasa.
Mugabe bado hajaapishwa kwa muhula wake wa saba akitawala Zimbabwe, kwa sababu ya kesi ya MDC mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
MDC kilisema kina ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa wizi wa kura ulitokea na kwamba kulikuwa na visa vingine vilivyohujumu matokeo ya uchaguzi huo ikiwemo, rushwa , dhuluma na kuvurugwa kwa daftari la wapiga kura.

NIMEIPENDA:::: KUTOMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO NI SAWA NA KOSA LA JINAI AMBALO HUKUMU YAKE NI "KUMWAGANA"












Ndoa yoyote ambayo mke au mume hafiki kilele hiki cha Mlima Kilimanjaro…,hiyo siyo ndoa inayokwenda sawa na kuna madhara makubwa kwa pande zote, kwa maana ya mwingine kuweza kuamua kutoka.
 

Ni vizuri walio kwenye ndoa kujifunza namna ya kupeana raha iwapasayo wanandoa kuipata. Kama unafikiri mkeo unaye kwa sababu amekuja kutafuta kula au kununuliwa magari na nguo, hilo ni kosa. Tafakari namna ya kupeana raha kwa kila kona.

 

Kama ni kula, kila mtu anaweza kujitafutia kwa njia mbalimbali kama ni kuuza mama ntilie na kadhalika.
 

Mwanamke yuko kwa mume kwa sababu anahitaji kupata vitu ambavyo wanawake huvipata kutoka kwa wanaume; …Mume ndiyo kichwa, iongoze ndoa yako vizuri kwa hekima; …Kichwa kikiwa ‘bangi’, ubavu (mke) atafanya nini?



Ni suala la lazima

Kwa asili, inatakiwa mke na mume kufanikisha zoezi hilo la kuwezeshana kufika kileleni  na  ni jambo muhimu kama ilivyo kutoka jasho mwilini, maana siyo tu mwili unaondoa uchafu ndani ya mwili, pia inasaidia kuupoza mwili kuwa sawasawa.


Najua wapo wanaoweza kusema aaah mbona mimi nimekaa mwaka sitaki tena mwanaume au mwanamke na sijapata madhara… Inawezekana ni kweli, lakini wengi hupata madhara.
 

Kadhalika kuna wengine wanafanya vitu vya hatari kama kutumia vitu mbalimbali kama mwanasesele (sex toys) au mashine maalumu zenye umbo kama la mwanaume au wengine kujichua au kusagana.

 

Ukidumu bila tendo la ndoa muda mrefu, baadhi ya madhara madogomadogo ni kama kuwa na hasira za mara kwa mara katika mambo madogo, hii hasa kwa wanawake ambao walishawahi kuwa na uhusiano unaokaribiana kuoana au waliwahi kuwa kwenye ndoa kisha wakatoka.

 

Kwa wanaume madhara yake ni kupendelea zaidi kuangalia picha za ngono. Kwa wote kwa maana ya wanaume na wanawake huwa na hali ya kusahausahau.


Kwa wanawake, wapo ambao hutokwa damu nyingi wakati wa hedhi. Kwa watu wote yaani wanawake na wanaume hupenda kurukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu) na wakati mwingine huongea kwa sauti ya juu hasa kunapotokea migogoro. 



 Wengine wana uwezo mkubwa wa kutukana au kutoa kauli yoyote unapomuuzi, anasema Leonard Trelawny katika jarida lake la mageuzi alilochapisha, New York Marekani.



Athari nyingine ni kuumwa na kichwa kwa wanaume na wanawake, kupoteza umakini katika kazi na kwa jumla sehemu za kazi wengi wa watu ambao wamesema hawataki tena kusikia mapenzi, siyo viongozi wazuri, wana kauli chafu, hata uamuzi wao mara nyingi siyo mzuri, ingawa siyo wote.



Hali kadhalika siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno. Aidha, unawaweza kuanzisha tabia nyingine mbaya kama ulevi, kukaa ofisini tu bila sababu.
Dismas Lyassa ni mtaalamu wa uhusiano aliyesajiliwa na Serikali kupitia taasisi ya Global Source Watch

-Mwananchi
 
 

KARIBU NYUMBANI FEZA KESSY,........ TULIKUMIS SANA


Hatimaye safari ya Tanzania katika Big Brother ‘The Chase’ imefikia tamati jana (August 11) baada ya mshiriki pekee aliyekuwa amesalia Feza Kessy kutolewa.


Feza ambaye amefanikiwa kudumu kwenye mchezo kwa siku 77 amekuwa mshiriki wa 20 kuliaga shindano hilo huku Cleo na Dillish waliokuwa dangerzone wakibaki salama.

 
Feza aliyekuwa ameshikilia bendera ya Tanzania wakati wa eviction hakuonekana kushtuka sana baada ya mtangazaji wa eviction show IK kumtaja kuwa ndiye anayefungasha mizigo, huenda kwasababu tayari alikuwa ameshakata tamaa ya kubaki toka wiki iliyopita.

 
Matumaini ya Feza yalionekana kufifia kuanzia eviction ya wiki iliyopita ambayo hakuamini kuona amebaki huku kipenzi chake Oneal akitolewa, lakini katika dairy session ya jana jioni masaa machache kabla ya eviction pia alisikika akimwambia biggie “I feel like it is over for me,” baada ya Biggie kumuuliza alimaanisha nini aliposema “I have lost hope but not in a bad way I think it is a defence mechanism”.
 
Nguvu ya ushindi kwa Feza ilianza kupungua siku kadhaa baada ya kuzama kwenye mapenzi na Oneal kiasi cha kuwafanya washiriki wenzao kuwaona wanajitenga muda mwingi na kujisahahu kuwa wapo mchezoni.

 
Moja ya maswali ambayo IK alimuuliza Feza baada ya kutoka ni kama bado anampenda Oneal, na jibu lilikuwa “Yes I do”, je unadhani hii inamaanisha kuna kitakachoendelea sasa baada ya ONEZA wote wawili kurudi katika maisha yao ya kawaida?


Baada ya Feza kuondolewa katika The Chase sasa Tanzania inaungana na Kenya na Uganda kubaki kuwa watazamaji baada ya washiriki wote wa Afrika mashariki kutolewa.


Nigeria ndio nchi pekee ambayo mpaka sasa washiriki wake wote wawli Melvin na Beverly bado wako mchezoni wakiwa ni miongoni mwa washiriki 7 waliosalia huku zikiwa zimesalia siku 13 kufika fainali. Unahisi nani ataondoka na $300,000 za Big Brother mwaka huu?

Saturday, August 10, 2013

NEW MNIMBO GENERAL ENTERPRISES LIMITED



NEW MNIMBO GENERAL ENTERPRISES LIMITED         

P.O BOX 105018  Dar es Salaam Tanzania 
Cell: 0767 203691   / 0784 20369   /  0719 965074 / 0754 309346



                                                          COMPANY -PROFILE 

new  mnimbo General Enterprises Limited  was established in 2011. It is situated in Temeke district Dar es Salaam .  New  mnimbo General Enterprises Limited has a reputation for its reliability of server delivery in engineering and fabrication industries. New Mnimbo General Enterprises supply precision tooling to the industries including Verniers standard, Dial and digital and specialized gear tooth micrometers standards and Digital and specialized.

Thread and bore, cutting tools including High speed steel and amp ; Solid carbide power saw Blades.

New Mnimbo General Enterprises Limited also supply a variety to tungsten carbide inserts to the manufacturing. New Mnimbo General Enterprises Limited tools include General hand tools, Workshop tools in including Hydraulic pneumatic and mechanic maintenance and  power tools.

PRODUCT & SERVICES 

>eletrical power transformers
>fasteners, bolt nuts ,rivets & washers 
> firefighting & rescue equipments
>footware
>General Eletrical Equipment 
>Greases
>Hose Fittings 
>Lifting taccle & attachment
>Hydralics & Pneuamatics 
>Machine tools 
> Material Handling Equipment 
> Non- Ferrous metals 
>.power tools
>Pulleys 
>Pumps 
>Safety Equipment & Clothing 
.>Tool die & Drill Steel
>Washing, Screening & Cleaning Plant Equipment 
>Welding & Flame cutting equipment
>Wire ropes & steel cables 
>Hardware
>Adhesives
>bearing 
>belting require sites
.>Boilers , steam generators & super heaters


SHEIKH APIGWA PANGA SWALA YA IDD



na Ibrahim Yassin

 SHEIKH Mkuu wa Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya Nuhu Mwafilango, ameshambuliwa na kujeruhiwa kwa panga baada ya kuzuka kwa vurugu katika msikiti mkuu wa wilaya ya Kyela. Vurugu hizo zilisababisha kujeruhiwa vibaya kwa watu wengine watatu baada ya kushambuliwa kwa mapanga na visu.

 Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Tanzania Daima kuwa vurugu hizo zinazoaminika kuwa ni za kugombea madaraka, zilizuka majira ya saa mbili asubuhi jana wakati sheikh huyo akiongoza ibada ya Idd el Fitri katika msikiti huo. Imedaiwa kuwa kundi la vijana likiongozwa na mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela (jina limehifadhiwa) alimshambulia kiongozi huyo kwa panga na kusababisha vurugu kubwa.

 Imeelezwa kuwa kikundi hicho cha vijana ambao baadhi yao wanadaiwa kukodiwa kutoka katika misikiti ya mikoa jirani, wakiwa na mapanga, nondo na visu walianza mashambulizi hayo, na ndipo wakakumbana na hasira za waumini wengine waliokuwa wamejiandaa kukabiliana na mashambulizi hayo. Mmoja wa vijana waliojeruhiwa vibaya kichwani ametajwa kwa jina la Hamis Hussein ambaye alipambana na vijana walioanza kumshambulia sheikh huyo. Imedaiwa kuwa kulikuwa na fununu za kuzuka kwa mapigano hayo, hatua iliyofanya uongozi wa msikiti kutoa taarifa polisi ambao walijipenyeza katika swala hiyo ya Idd.

 Wengine waliojeruhiwa vibaya ni mmoja aliyetajwa kwa jina la Magogo anayetuhumiwa kuchochea vurugu na mapigano hayo katika kile kilichoelezwa jitihada za kuwaondoa viongozi walioko msikitini na kuwadhamini vijana ambao wanadaiwa kuwa ni waasi wa msikiti huo.

Akizungumza na Tanzania Daima Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Kyela Daud Mwenda alisema kuwa kikundi hicho kinapingana na uongozi uliopo msikitini hapo hivyo wanataka kushinikiza waumini wengine waupindue uongozi uliopo. Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela ambaye hakutaka kutaja jina lake alikiri kupokea majeruhi watatu waliotokana na vurugu hizo. Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Unyakyusa Helly William alisema kuwa ofisi yake imepokea taarifa za vurugu katika msikiti huo na kudai kuwa jambo hilo limewasikitisha sana kama viongozi wa serikali.

William alisema msikitini sio mahali pa kufanyia vurugu bali eneo takatifu linalotumiwa na watu kumuabudu Mungu.
RESPECT TANZANIA DAIMA

Friday, August 9, 2013

BREAKING NEWS:::: MILLIONI 10 KWA ATAKAE FANIKISHA KUKATWA KWA WAHUSIKA WA TINDIKALI ZANZIBAR......





Polisi nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa watu waliowashambulia wasichana wawili waingereza kwa Tindikali.
Wasichana hao kutoka London, Kirstie Trup na Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa wanatembea mjini Jumatano Jioni.

Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.
Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo.
Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.
Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.
Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote. Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.
Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njema.

'Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' alisema msemaji wa familia za wasichana hao.
Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.
Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa kampuni ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali yao si mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo vimewahi kushuhudiwa vya kuchomwa kwa Tindikali
Msemaji mwingine aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa shambulizi hilo.

Thursday, August 8, 2013

HII KALI: WANAUME WA KIAFRIKA WANAONGOZA KUWA NA UUME MKUBWA....





Kwa sababu ambazo binafsi sizielewi, mwanasayansi mmoja kutoka nchini Ireland aliamua 

kufanya “utafiti” wa kulinganisha wastani wa ukubwa wa uume wa watu wa nchi mbalimbali. Alifanya utafiti huo kwa kulinganisha mataifa 113, ambapo wanaume wa Afrika ndio waliongoza kwa ukubwa na Waasia walikua wa mwisho.


Utafiti huo ulifanywa na Profesa wa saikolojia, Richard Lynn, wa Chuo Kikuu cha Ulster na utachapishwa katika jarida la kisayansi la Personality and Individual Differences. Profesa huyo alisema matokeo ya utafiti wake yamethibitisha nadharia ya awali kuhusu mahusiano ya urefu wa uume, ya kwamba Negroids(watu weusi) ndio wanaoongoza kwa ukubwa wa wastani wa uume, na Mongoloids (Waasia) ndio wana wastani mdogo kuliko watu wote.


Top 4 kati ya nchi zote 113
1. Congo ndio wanaoongoza kwa urefu wa wastani wa uume ambao ni inchi 7.1
2. Ecuador kwenye wastani wa inchi 7.0, 
3. Waghana inchi 6.8; na 
4. Raia wa Colombia inchi 6.7.


Katika wanaume wa Ulaya, 
1. Wataliano ndio walioongoza na wastani wa inchi 6.2
2. Ugiriki inchi 5.8 
3.Ujerumani inchi 5.7
4. Waingereza inchi 5.5 , na 
5. Wafaransa, inchi 5.3
Walioongoza kwa udogo katika mataifa yote yaliyofanyiwa utafiti ni Korea zote mbili (Kaskazini na Korea ya Kusini) ambao wote kipimo chao, ni wastani wa inchi 3.8. 
Swali je Tanzania tupo wangapi?


USHAHIDI

DIVA WA CLOUDS FM TENA......... "SIJAWAHI ONA MWANAUME MZURI KAMA PREZZO HAPA DUNIANI"

Kwa  mara  nyingine  tena,  mtangazaji  wa  Clouds fm  maarufu wa  jina  la  DIVA  amejitosa Istagram  na  kuanza  kuisifia  suruali yake ( Prezzo)  huku  akiwaponda  wanaume  wa  kibongo  na  wale  wote  wanaomchukia  Prezzo....


HUU NDO UJUMBE WAKE KWENU

“The way my heart beats for u Mentiond of your name, One touch never enough you driving me Insane, swing me take you back, who am i to blame but myself, need you back in my life simple and plain, Crazy nights arguments running towards the door, lying to myself that I don’t wanting you no more. 


"No matter what we been through You’re the only man that I adore… you are the only one I need in this world.. see People use to tell me I was Crazy, told me not to give in, told me that you would never love me all I did is pretend.

"I told them to mind their business Cause they are not in my Position… when I said I was in love… they said with that UGLY face ‘ girl you tripping… 

"I cut the negativity cut the haters off and I got into my man… coz I take him for all he is.. and he takes me as I am. 


"The way I feel about him is God’s Perfect plan. Everyone know I am his girl……he is the Only One I need. habari ndio hiyo. Sibadiliki and haachwi mtu.”

EID MUBARACK...................

Team Truth inawatakia Watanzania wote Eid MUBARACK AMANI NA UPENDO VIWATANGULIE WOTE..........

Wednesday, August 7, 2013

NGOMA MPYA: MABESTE ft PETER MSECHU - NISHAURI DOWNLOAD HAPA

DOWNLOAD HAPA

SABABU ZA KIBIASHARA ZAIHAMISHIA BONGO STAR SEARCH (BSS) TBC1!!!!!!

Epiq Bongo Star Search ya mwaka 2013 haitaoneshwa tena kupitia ITV. Mwaka huu shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba litakuwa likioneshwa kupitia TBC1. 


Kupitia Facebook, Rita Paulsen aka Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa sababu mbili za kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1.


“Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1. 


Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving’amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.”

Monday, August 5, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU: KWA VIGEZO HIVI KIDUME UTAPENDWA TU!!!!!!!!!!!!





Jana kulikua na kikao cha dharura na cha ndani ya TEAM TRUTH ambapo moja ajenda ilikua ni kunipongeza mimi (TEAM TRUTH 18+) kwa kazi nzuri ninayo ifanya na kwa ratiba ilikua nimalize session hii ya mapenzi jumatatu ila nikapewa muda zaidi hivyo kuamua leo kudondoka na hii kwa ajili ya mabrother wenzangu............................


watu wengi wamekua wakitafuta jinsi gani wanaweza kupendwa na wasichana au wanawake na ni wazi kila mwanamke ana chaguo lake kwa mwanaume ampendae huendaa ukawa na vigezo kibao na bado akapenda vigezo vichache na ukabaki unashangaa why kantosa?

KWA MSAADA TEAM TRUTH 18+ NIMEAMUA KUDONDOKA NA VIGEZO 10 AMBAVYO NI KIVUTIO KWA WASICHA AU WANAWAKE WENGI.....................................................

wengi watajiuliza why not pesa? jibu ni rahisi sana imetokea mara nyingi mtu akapendwa tu bila kujali pesa na watu pia wakashangaa mbona hata sura hana? mchunguze mtu huyu kuna kigezo lazima kakuzidi na ukikigundua BELIEVE ME YOU WILL ALWAYS STAY CONNECTED WITH GIRLS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

1) kuwa na malengo yote ya muda mfupi na mrefu katika maisha yako na misimamo isiyo tingishika.

2) mwenye kujiamini.

3)mwenye kutunza siri na si mropokaji ovyo.

4) mcheshi (na hii kivutio kwa wasichana walio wengi)

5) hisia na uadilifu.

6) mwenye kusamehe tena na kusahau.

7) mwenye kujithamini.

8) mwenye utashi na upeo wa mambo.

9) huruma na heshima kwa wote wadogo na wakubwa

10) mwenye hadhi na mtanashati katika mambo yake ikiwemo uwezo binafsi wa upembuzi wa mambo.


Sunday, August 4, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU; USAGAJI (lesbianism) KWA WANAWAKE NA SABABU ZAKE. (VERY SENSITIVE IN TANZANIA HASA KWA MASTAAA)


SAMAHANI KWA PICHA HII

Usagaji (lesbianism) ni tabia ya wasichana/wanawake kujiridhisha kimapenzi wenyewe pasi kuhitaji kuridhishwa na mwanaume. Wasichana hawa hutumia vidole, ulimi na hata sex toys (dildo) kama zana wakati wa kufanya tendo hilo. Wengi wa wasichana wanaojihusisha na tabia hiyo hufurahia zaid tendo hilo tena kuliko hata wakifanya na wanaume na hivyo kuwafanya wajione kwamba hawana sababu ya kuwa na partners wa kiume. Zifuatazo hapa chini ni sababu ambazo kwa mtazamo wangu ambazo naziona ndio sababisho la wasichana wengi kujiingiza kwenye tabia hii na hata kuona ndiyo maisha yao.
Sababu hizo kwa mtazamo wangu ni hizi hapa

• Kuiga kutoka kwa wenzao: wengi wa wasichana ambao wamejikuta wanatabia hii wameiiga kwa wenzao, hasa wanapokuwa kwenye eneo ambalo wapo wenyewe kama vile shule hasa za bweni na maisha ya hosteli. Wasichana wengi ambao walisoma shule za bweni ama kuish maisha ya hosteli walijikuta wanafundishwa tabia hii na wenzao ambao tayari walikuwa wameshaanza tabia hizi toka kabla ya kuja shule. 


 Kutaka kujiexplore: kwa kawaida watoto hupenda kujiexplore viungo vyako, yaani watoto wakiwa wadogo hutaka kujidadisi wawe wa kiume ama wa kike. Mfano mzuri watoto wa kiume wanapokuwa pamoja hata wakioga hujikuta wanachezeana sehem zao za siri hadi uume unasimama, like wise watoto wa kike hupenda kujidadisi kwa kucunguliana sehem zao za siri. Tabia hii kwa umri wa udogo huwa haina neon manake khuishia hapo lakini wapo wachache ambao tabia hii hawaiachi huiendeleza hadi ukubwani na hivyo kuwa ni sababisho la kujiingiza kwenye same sex plays.

• Hormonal make up: hii hutokana na jinsi binti alivyzaliwa. Kuna baadhi ya mabianti ambao wamezaliwa na hormone za kiume na hivyo kujikuta kwamba wanatabia za kiume. Wengi wa mabinti ambao wana tabia hizi kwenye mashule ya bweni huwa na desturi ya kuoa na hivyo kuitana mume na mke na wao huwa na tabia za kukaa kimapenzi mapenzi na hwa wanaowaita waume ama wake. Wasichana kama hawa huweza kuwashawishi sana wale ambao ni wasichana wa kawaida hadi kujikuta wanaanza tabia hii ya kusagana wakiwa mashuleni na wakisha ianza basi huwa siyo rahisi kuiacha mpaka nguvu nying zimetumika kumfanya aache.


• Raha itokanayo na tendo lenyewe: wengi wa wasichana /mabinti wanaoshiriki tendo hili huwa wanadai wanaridhika sana kimapenzi wanapofanya hivi ukilinganisha na wakiwa wanafanya na wanaume. Kutokana na tabia hii wengi wa wanwake ambao wako kwenye mahusiano ya kindoa hujikuta wanafanya hii tabia ili tu kuridhika kwasababu wanapofanya na jinsia ya kiume hawaridhiki.

• Maudhi ya mahusiano ya heterosexual, maudhi yatokanayo na mahusianoa ya jinsia mbili huwa yanawakinai wengi wa wasichana/ wanawake na hivyo kugeukia upande wa pili ambapo wanaamini kwamba hakuna maudhi hayo. Wanajua wazi kwamba wakiwa wenyewe watabembelezana, na kupeana raha zisizokuwa na maudhi.



• Umbali kutoka walipo wenzi wao: kuna tabia ambayo imeibuka siku hizi na kwa masiksitiko makubwa sana inafanywa na wanawake ambao wenzi wao wako mbali nao. Baadhi ya wanawake ambao waume zao wako mbali nao kwa mauda mrefu wamejikuta wakiwa na mahusiano na jinsia moja kwa kigezo kwamba hawataki kuwasaliti waume zao. Na kwamba wanataka waume zao wakirudi wawakute hawajatumika kabisa. Sikatai usaliti ni mbaya lakini hata huu wa jinsia moja nao ni usaliti tu.

Ikumbukwe kwamba mahusiano ya jinsia ya aina moja haimaaniash kwamba hayana maambukizi ya magonjwa kama HIV/AIDS and the like hivyo yeyote anayefanya hivi kwa kigezo kwamba anataka kujikinga na magonjwa anajiongopea na kwamba chances za infection huwa kubwa tu.


Pia ni kujidanganya sana kusema kwamba mapenzi ya jinsia moja ama ya usagaji ni matamu sana kwani huwa mwanaume akifundishwa kufanya kama vile ambavyo mwanamke msagaji anaweza kufanya basi mapenzi haya yatakuwa na raha kama kawaida. Haina maana kwamba mwanamke tu ndio anayeweza kutumia ulimi wake ama kidole chake ili kumpatia mwenzie raha, ila hata mwanaume pia anaweza kutumia vitu hivi na hivyo kumpatia raha mwenzie.

Pia tabia hii ya usagaji kwa wale ambao wanaifanya hasa pale waume zao wanapokuwa safarini, eti kisa wanataka waume wakirudi wawakute hawajazini wanajidaganya sana kwani kusagana na kuzini kwa kawaida kote ni kuzini hata kama hukuingiziwa kitu ndani ya uke. Kinacho determine kutokuwa mwaminifu ni kitendo cha usaliti iwe umezini na mtu mume ama mwanamke mwenzio. Hivyo usidanganye nafsi yako kwamba huwez kuzini na mwanaume kisa utamsaliti mumeo, ukasahau kwamba hata na huyo mwanamke mwenzio pia ni usaliti.

reference

Saturday, August 3, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU : SABABU KUU ZA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA / MAPENZI (KUJAMIIAANA)

Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano wa mwanamke na mpendwa wake. Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana sana kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.
Visababishi vya tatizo hili kwa wanawake ni;

  • KUSAGANA AU MAPENZI YA JINSIA MOJA KWA WANAWAKE.

  • Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili linaweza kutokea kutokana na msongo wa mawazo ambapo huchangiwa na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa uaminifu katika uhusiano {infedility} nk) na magonjwa mbalimbali.
  • Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au ndoa
  • Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana kwa kuingiliana na ufanyaji kazi wa homoni/kichocheo chengine kinachojulikana kama dopamine (ambayo ndio humfanya mtu kufikia kilele wakati wa kujamiana). Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu nyengine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo (anterior pitituary tumors). Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume(impotence).
  • Kupungua mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
  • Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
  • Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu
  • Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote hupunguza hamu ya kujamiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Uvutaji sigara
  • Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
  • Uzito uliopitiliza (obesity)
  • Ugonjwa wa mifupa (arthritis)
  • Utumiaji madawa ya kulevya
  • Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve damage) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
  • Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu,antidepressant medication, dawa za saratani nK.
  • Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo kusababisha uchovu.
  • Ugonjwa wa moyo
  • Saratani ya aina yoyote ile
  • Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression nk.
  • Historia ya kubakwa, au kupata maumivu wakati wa kujamiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari kujamiana au kutotayarishwa vyema kabla ya kujamiana au magonjwa ya zinaa.
  • Tatizo la vaginismus – Hii ni tatizo ambalo husababisha tupu ya mwanamke kuwa ndogo wakati wa kujamiana na hivyo husababisha mwanamke kupata maumivu wakati wa kujamiana.
  • Kupenda intaneti kupita kiasi (addiction) – Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchat au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababishwa msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.
Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?
  • Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
  • Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
  • Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (menopause- miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri nadepression.

Friday, August 2, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU: MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO




ATHARI za PUNYETO
Wanaume waliowengi hukidhi haja zao kwa kutuliza matamanio yao kwa njia ya kujichua/ kupiga punyeto bila kufahamu madhara yake: Nikweli punyeto inasaidia kupunguza hamu ya tendo na ni njia nzuri ya kujiepusha na zinaa kwa kujilinda na maradhi ila kiukweli ina madhara na madhara yake mara nyingi hutokea kwa mtu anaependelea sana kupiga punyeto, kutokana na utafiti uliofanywa kisayansi imeonekana punyeto ni nzuri kiafya ila endapo kama utakuwa unapiga mara moja moja na sio kila siku. Napenda kuwashauri watu wanaopiga punyeto wawe makini na wasiendekeze jambo hili kwani madhara yake ni makubwa sana na Athari zake kubwa ni hizi zifuatazo:

1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME:
Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inaregea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umeregea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO:
Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya mapenzi na mpenzi wake na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mpenzi wake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kusex.

Athari nyingine ni kama zifuatazo 

3.Uchovu wakati wote 
4.Maumivu ya nyonga 
5.Kusinyaa kwa Nywele/Nywele kunyonyoka 
6.Maumivu ya kende 
7.Maumivu ya kiuno 

Mpendwa wa safu hii hizo ni athari kuu 2 tu, ingawa ziko nyingi ila hizi nilizozitaja ni kwa uchache na ndio zinazo wakumba wanaume walio wengi. Ushauri wangu mimi kama wewe unapiga punyeto basi jitahidi usiwe unapiga kila siku atlist kwa wiki mbili mara moja endapo kama utajisikia hamu ya kusex kama huna mpenzi au ukishindwa acha kabisa.

Thursday, August 1, 2013

SOMA NI MUHIMU SANA SANA NA INASIKITISHA: KANSA YA NGOZI YAMHARIBU MTOTO WA MIAKA 7 VIBAYA SANA....

MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.




“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.

“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi. 

REFERENCE

JOINT MPYA: OMMY DIMPOZ ft J MARTIN - TUPOGO DOWNLOAD IT HERE

DOWLOAD IT HERE

NU JOINT: NEY WA MITEGO ft NEYBA - SALAMU ZAO............. DOWNLOAD

DOWLOAD HAPA