Sunday, July 28, 2013

SIKILIZA NA DOWNLOAD NEW HIT "VAN B ft TCHAZ - LAWAMA"



BOFYA HAPA KUDOWNLOAD.

PEREMENDE MUSIC EMPIRE IMEPOKEA VIFAA VIPYA "KEEP IN TOUCH"


Recording label "peremende Music Empire" yenye maskani yake mjini Dodoma imepokea vifaa vipya vya production kutoka UK, akiongea na TEAM TRUTH  the CEO Erick Backamaza amethibitisha hilo na kuwataka watanzania kujiaanda kwa project tu.
................." sa ivi ni mawe baada ya mawe nimepokea vifaa vipya kutoka mbele na sasa tupo katika project ya kutengeneza muvie inayoitwa "40 DAYS" hivyo watanzania kaeni mkao"............ amen ma men.......
kwa sasa peremende ndo label inayo fanya vizuri zaidi kutokea Dodoma... kila la heri katika mafanikio yenu.

LULU: "SIKU HIZI NASALI NA NAMUAMINI MUNGU NATAMANI NINGEISHI HIVI NYUMA".





MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. 


Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza

KAULI NZITO: TEAM TRUTH LIVE KATIKA KONGAMANO LA MUSTAKABALI WA AMANI NA USALAMA WA TAIFA LETU KWA MIAKA 50 IJAYO UDSM.




 HAYA NI BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA KATIKA KONGAMANO HILO KATIKA RED NA MAJINA YA WACHANGIAJI (team truth inaomba radhi endapo majina haya yamekosewa) 

Chama kilichoko madarakani kisiwe chama dola ili kuleta usawa…………… PROF. Mpangala Gaudence. 

Tutauawa sana… Tutafungwa sana… Tutaonewa sana kwa sababu mfumo unaoendesha nchi umeparaganyika……………. MH. Tundu lisssu

Liliani Wasira………….. ( mwanasheria) tusitafute mchawi tunamjua na ni serikali kulewa madaraka na watanzania kuwa waoga. wanaume lazima mthubutu msiwe waoga MH. PINDA karahisisha kwamba serikali imechoka na fimbo ya mnyonge ni kura.

IDDI MAJUTO,……………. wanasiasa wa tanzania wanajuana na lao ni moja na ndo mana wancheza mziki pamoja hivyoikitokea vita mtanzania wa kawaida ndie atake umia

MIGOMO ELIMU YA JUU……….. FAHAMI… vyombo vya habari vinapotosha ukweli kuhusu migomo elimu ya juu.. waziri mkuu katupilia mbali mapendekezo 16 kuhusu migomo. viongozi kukaa kimya hasa muheshimiwa raisi ni uoga wakuwakabili wasomi.

MAYROSE… (MWANAHARAKaTi WA MAENDELEO)… kiongozi ni taa nimtu wa kuonesha njia …waziri mkuu mtoto wa mkulima amekidharau kilimo kwamba ni duni,

 Dr. SLAA. mchawi wetu hayuko nje ni serikali huku akionesha waraka mballimbali ikiwemo tume mbalambali zilizoundwa, tume ya haki za binadamu imetoa taarifa ya mauaji na serikali imeificha, jeshi linapoteza hadhi (huku akiomba radhi) serikali nitatizo la ardhi, elimu ni duni tatizo ni serikali

MWAKILISHI NCCR MAGEUZI…. nguvu ya hoja ndo siasa ya nccr na si kulalamika.

PILLI SAIDI (MWANAHARAKATI)… maandamano ni haki ya kikatiba.. baadhi ya yama vya siasa hutumia maandamano na vijana kutekeleza matakwa yao hivyo serikali iwe na njia mbadala ya vijana kujiajiri kuepusha maandamano yasiyo lazma. vyombo vya habari vitumie busara katika kulinda amani ya nchi kwani wanaoumia ni sisi.

AMAN MUHONJWA (MUHITIMU UDSM)……… tanzania haina amani bali utulivu tu huku akitaja matukio baadhi ikiwe lile la mabomu, miaka 50 ijayo ni giza huenda wajukuu zetu hawatoiona amani kabisa

BW. JUSTIN………..watanzania tufikiri tuko wap, utele na kufikika vinahitaji uongozi bora. polisi wanafanya kazi nzuri na wanaweka uzazi wa mpango na kosa la jinai halifichiki ipo siku utakuja na utahukumiwa

JENERALI….. hakuna vitendo vya ubakaji mtwara hizo ni propaganda zinazo katisha tamaa na si kila mwana siasa angependa kuiona hali ile mtwara (amani) NAIBU KATIBU MKUU CUF…… hali ya amani inavunjwa na vyombo vya dola vithibitisho vya ubakaji mtwara vipo na kamshangaa jenerali kukanusha.

KATIKA HILI NAPE NAUYE UNAKOSEA: "WALIOPENDEKEZA SERIKALI TATU NI WAZEE WANAOSUBIRI KUFA"

MZIMU wa serikali tatu bado unaendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo jana, Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipinga tena uwepo wa serikali tatu na kudai kuwa waliotoa maoni hayo ni wazee wanaosubiri kufa. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili mchakato wa Katiba Mpya, katika ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye alisema nia ya serikali tatu ni kuleta matabaka ambayo yatasababisha migogoro. “Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja Muungano enzi za ujana wao? Wamenufaika na Muungano kwa kipindi cha miaka 50, sisi vijana wanataka kutuachia mgogoro!”alisema Nnauye. Nape alisema kuvunjwa kwa Muungano kutasababisha mgogoro mkubwa wa rasimu kutokana na muda ambao Muungano huo umedumu. Alisema kuundwa kwa serikali tatu si sera ya CCM kama wanavyodai wapinzani, bali ni maoni ya watu waliyoyawasilisha katika ukusanywaji wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya. “Sera ya CCM ni kuongoza serikali mbili na si tatu, na hii sera tutaendelea kuitetea na kuilinda mpaka mwisho wa dunia, tunachoamini katika chama chetu hatuogopi kutetea sera ambazo tumezitoa wenyewe,” alisema Nnauye. Alisema ni vyema zikamalizwa kasoro zilipo katika mfumo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na si kuongeza madaraka yasiyo na tija. Nape alisema kitendo cha Tume ya Jaji Joseph Warioba kusema imetumia sheria ya mwaka 1964 kuwa kigezo cha kuundwa kwa serikali tatu si sahihi, kutokana na makubaliano ya mwaka huo kwamba ni serikali mbili. Kiongozi huyo wa CCM pia alishangazwa na kitendo cha Rasimu ya Katiba mpya kutamka wazi idadi ya mikoa pamoja na wilaya ambazo zitatumika katika uchaguzi na kwamba mwenye jukumu hilo ni Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. “Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa serikali tatu itaelea katika madaraka, kwani serikali ya Tanganyika itakuwa haiwezi kuwatetea wananchi, hali itakayosababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa urasimu ambao ni adui wa maendeleo,” alisema Nnauye. Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa Muungano kutasababisha kuiburuza Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani asilimia 95 ya uchumi wa visiwani unategemea Tanzania Bara. Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa kiongozi ni kuwatetea wananchi na si kuwazidishia mizigo. Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Nnauye alisema CCM hakiogopi mgombea binafsi, kwani hata akigombea chama hakitapata hasara yoyote. Nape alisema sera ya CCM ni kukataa wagombea binafsi wanaouza unga na si kukataa mgombea binafsi kama ambavyo vyama vingine vya siasa vinavyodai katika vyombo vya habari. Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9 inazungumzia umri wa Mbunge kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa CCM suala hilo si sahihi, kwani wabunge wenye miaka 21 wanawajibika vizuri kuliko wazee. Mtanzania

SIKILIZA NA DOWNLOAD CentalZone - Tukutane bank



BOFYA  HAPA KUDOWNLOAD

Saturday, July 27, 2013

DOWNLOAD NA SIKILIZA NYIMBO YA CLIMAX - UJUZI

BONYEZA HAPA:
http://www.hulkshare.com/w9mm55kl3sw0

MISRI HALI SI SHWARI INASEMEKANA NI HALI MBAYA ZAIDI KUWAHI KUTOKEA TANGU RAISI ANG'OLEWE MADARAKANI.

Daktari katika hospitali ya muda amesema watu wawili walifikishwa wakiwa kichwa na viwili wili vyao vimetenganishwa huku wengine wakiwa na matundu ya risasi vichwani na kifuani.Muslim Brotherhood wamelilaumu jeshi kwa kuwapiga risasi na kuwauwa wafuasi wao.Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi wamesema zaidi ya watu laki moja na ishirini wameuwawa katika mapambano na vikosi vya ulinzi na usalama mjini Cairo.

Polisi waliingia katika mkusanyiko wa usiku wa wafuasi wa Morsi saa chache baada ya waziri wa mambo ya ndani kusema wafausi wa Morsi na chama chao cha Muslim Brotherhood waliokusanyika kwenye viunga vya msikitini wa Rabba Al Adawiya lazima waondoke.
Hospitali hiyo imekuwa katika hali ngumu ya kumudu miili ya marehemu na majeruhi wanaofikishwa hospitalini hapo.
Mwandishi wa BBC anasema ni mapigano mabaya zaidi tangu jeshi limuondoe rais Morsi madarakani.
Wakati huo huo, Uingereza imekemea matumizi ya nguvu yanayopoteza maisha ya watu nchini Misri.
Waziri wa masuala ya kigeni William Hague amewataka wenye mamlaka kumaliza mapigano na vurugu hizo.
Amesema wale waliohusika na mauaji hayo ni lazima wawajibike na haki ya wanaoandamana kwa amani ni wajibu ilindwe.
Bwana Hague pia amelitaka jeshi kuwachilia huru viongozi wa Muslim Brotherhood waliowekwa kizuizini akiwemo rais Mohamed Morsi.
via BBC SWAHILI

Friday, July 26, 2013

KWA UFAHAMU ZAIDI KUHUSU SHERIA ZA KAZI TEMBELEA LINK HII NA DOWNLOAD (attachment).


http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-sheria-the-law-forum/24624-tanzania-labour-law-sheria-ya-kazi-tanzania.html

KIKWETE: IGUSE TANZANIA UKIONE CHA MOTO.... WATANZANIA LALENI KWA AMANI.


RAISI JAKAYA KIKWETE ametuma ujumbe kwa wale wanaoitisha tanzania. amewaambia wakithubutu watakiona cha mtema kuni kama ilvyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda
Alisema mamlaka za ulinzina usalama zilimdhibitiAmin alipofanya uvamizi katik ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingineyeyote atakaechezea usalama wa nchi. 

Wakati raisi akiyasema hayo, Mkuu Wa Majesh, Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wowote jeshi lipo imara na kuwataka wasiogope lolote.
Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya iliyopo Muleba, Kagera.
“Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wakati wowote, saa yoyote tuko tayari kulinda nchi yetu. Hatuko tayari kuona amani inaharibika nchini, hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kuimega au kuichezea nchi yetu kama alivyofanya Idd Amin.”Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanzania.
Jenerali Mwamunyange alisema jeshi wakati wote liko imara kuwalinda wananchi na nchi kwa jumla hivyo wasiogope...“Endeleeni na shughuli zenu na msiogope mtu yeyote, fanyeni kazi zenu bila wasiwasi.” Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo, Jenerali Mwamnyanye alisema yeyote atakayethubutu kuchezea usalama wa nchi atakiona cha mtema kuni. Akizungumzia Siku ya Mashujaa, Rais Kikwete alisema ni siku ya kuwakumbuka mashujaa waliojitolea maisha yao wakati wa Vita ya Kagera kuilinda nchi yao ili iwe salama na yenye amani. 
“Kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama yake kwani kuna wengine walikufa na wengine wakabaki na vilema kwa ajili ya hilo. Wale ambao wamebaki na wana matatizo lazima tuwaangalie vizuri na vile ambavyo havijafanyika tutavishughulikia kwani kutetea taifa ni kazi ngumu.”
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu ambao wote walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Awali, viongozi wa dini, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini, Shehe wa Mkoa, Haruna Kichwabuta na Mwakilishi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo, Askofu Elisa Buberwa walitoa wito kwa Watanzania kuthamini amani iliyopo na umuhimu wa kuwa na mshikamano katika kuilinda na kuhakikisha kwamba haivurugwi kwa misingi ya imani, itikadi au ukabila.
Matatizo Muleba
Awali, Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi wa Muleba kuwa matatizo ambayo wabunge wao wameyawasilisha kwake mbele yao atayashughulikia.
“Nimesikia yale waliyoyasema hapa ; suala la mpaka kati ya eneo la wananchi na jeshi, Waziri wa Ardhi yupo hapa, kaeni na jeshi na vijiji ili tatizo liishe ni jambo ambalo linawezekana hivyo litatuliwe,” alisema Rais Kikwete.
Alisema suala la umeme na madaraja litashughulikiwa na viongozi wa mkoa wakishirikiana na wabunge na watakapokwama wafikishe kwake... “Mimi ndiye ninayetoa fedha za maendeleo hivyo hayo masuala yakikwama waniambie nitayashughulikia.” Chanzo: Mwananch

HURUMA MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTER: HII NDIO HALI YAKE BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI.

MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

 Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

 Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki. Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua. Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni. Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake