mmoja anayekadiriwa
kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 amekutwa amekufa katika makaburi ya
Majengo soko la mjini Kahama mkoani Shinyanga huku mwili wake ukiwa ametobolewa
macho na kuonesha kupigwa na kitu kizito usoni.
Mwanamke huyo ambaye
hajatambulika jina lake na anakotoka alikuwa amevaa Blauzi nyeusi yenye madoa
meupe, viatu vyenye urembo wa silva, mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu.
Mwili wa Mwanamke huyo
amegunguliwa leo majira ya saa sita Mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba
kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa Polisi.
Kwa mujibu wa majirani wanaoishi
eneo la makaburi hayo, tukio hilo linakisiwa kutokea usiku wa kuamkia jana huku
baadhi ya kina mama wakisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke akipiga mayowe katika
eneo la mnadani.
Naye mwenyekiti wa kitongoji
cha Majengo Kaskazini Noel Mseven
amesema amepata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kufika katika eneo hilo
walibaini kuwa sehemu za siri za mwanamke huyo ziliingiziwa kitu chenye ncha
kali.
Jeshi la Polisi wilayani
Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Mrakibu msaidizi wa Polisi
Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti
ili kuutambua mwili huo.