Lilikuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Arusha, lilipata ajali maeneo ya barabara ya Chalinze- Segera Bagamoyo. Abiria wawili wamefariki dunia na wengine 63 wamejeruhiwa na kulazwa katika vituo vya afya kadhaa, zahanati pamoja na Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani baada ya basi mali ya Kampuni ya Meridian kuacha njia na kupinduka jana katika Barabara Kuu ya Chalinze- Segera wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
Abiria waliofariki ni miongoni mwa majeruhi 24 wa ajali hiyo ambao walipelekwa moja kwa moja kupata matibabu katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi baada ya hali zao kuonekana ni mbaya zaidi ya wengine katika eneo la tukio. Wengi walikuwa wamevunjika sehemu mbalimbali za miili yao.
Kamanda wa Polisi Pwani Ulrich Matei alithibitisha kutokea ajali hiyo.
Akizungumza hospitali hapo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya hiyo, Dk Peter Dattan alithibitisha kupokea baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya 24 waliofikishwa hapo wawili walifariki na wote ni wanaume majina yao bado hayajajulikana.
Dk Dattan alisema majeruhi 22 wanaendelea kupatiwa
matibabu na kati yao wanawake ni 12 na kwamba kwa jumla hali zao wote
ni mbaya kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata.
Naye Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Chalinze
walikolazwa majeruhi wengine Dk ,Victor Bamba akizungumza kituoni hapo
alisema majeruhi waliofikishwa hapo ni 12.
Alisema majeruhi watatu kati ya hao walikuwa wakifanyiwa mpango wa kupelekwa Tumbi baada ya hali zao kubadilika na kwamba wengi wao wameumia zaidi sehemu za kichwani, kuvunjika miguu, mikono na mbavu
Dk Bamba aliiomba Serikali na wadau wa afya
kuhakikisha kuwa utoaji na usambazaji dawa na vifaa tiba unalenga kwenye
maeneo yenye ajali nyingi za barabarani ili kuweza kupatikana dawa na
vifaa tiba kwa wakati pindi inapotokea matukio ya ajali.
Kwa mujibu wa mashuhuda na wakazi wa Kijiji cha
Kimange, Hamis Shaaban na Yusufu Mzee walisema ajali hiyo ilitokea saa
5.40 asubuhi jana
mwananchi.
mwananchi.
No comments:
Post a Comment