Saturday, August 31, 2013

Sumu ya nyuki inavyoangamiza VVU

USIFANYE HIVI NI PICHA TU

Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi.

DIAMOND ONCE AGAIN:DIAMOND NA LINAH WANASWA WAKITOMASANA HADHARANI


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
  

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
 

Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.


Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
  
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.

AIBU NYINGINE:::::IGP aibiwa upanga wa dhahabu



Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.

SOMA ZAIDI

Thursday, August 29, 2013

TEAM TRUTH 18+:::: JINSI YA KUFIKA KILLENI MAPEMA KWA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA.


Kama ambavyo wengi tunatambua kuwa sehemu kubwa (asilimia 99.5) ya kufurahia ngono ni Mapenzi ya kweli juu ya mpenzi wako ikisaidiwa na utundu wako wewe mwenyewe manamke na sio mwanaume japokuwa baadhi ya wanawake hutegemea wanaume wawafanyie kila kitu mpaka kuwafikishe.

Wakati mwingine wanaume huchoka kwa vile kwa kawaida wanawake tunachukua muda mrefu zaidi kufikia mshindo ukilinganisha na wanaume, kwamba mwanamke anafika ndani ya dakika 10-15 wakati mwanaume anafika ndani ya dakika 1-5 unless awe anajua kujizuia nahapo ndio atakwenda mpaka dakika 45 na baadhi huondoka zaidi ya hapo kutokana na kutosisimuliwa vilivyo (yaani akikupanda hamalizi mpaka uke unakauka na wewe hamu inakuishia) hahahahaha!


Well, back to topic......


Mbinu ya kuita kilele sio ngumu kama wengi mlivyokuwa mkifikiria/dhania bali ni ya kawaida sana na utashangaa ni jinsi gani inafanya kazi, na ikiwa umebahatika kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kujizuia basi unaweza kupiga 3 ktk mzunguuko wa kwanza.


Unapokuwa ukifanya mapenzi hakikisha akili yako yote iko kwenye kufanya mapenzi, sio lazima umfikirie mpenzi wako bali unaweza kufikiria chochote kitakacho kufanya "unyegetuke" zaidi wakati "mzigo" uko ndani ya uke sio.


Mfano unaweza kuwaza/kujisemea "nat......... sasa", unaweza kumuuliza mpenzi wako akuambie anafanya nini in rude way (it works 4 me), au kama anakujua vizuri basi anaweza akaanza kusifia Uke wako ulivyo, anavopenda kukufanya n.k (wengine nasikia huomba kutukaniwa wazazi wao.....hey it works 4 them so jaribu na wewe)


Jinsi jamaa anavyokufanya wewe pia msaidie.......well jisaidie na hakikisha unahangaika kupata "kipele" (mahali unaposikia raha zaidi pakiguswa), ukisha hisi mwambie atulie hapo hapo na wewe anza kufanya "makaratee" zunguusha kiuno chako ktk pembe zote (badilisha mirindimo) na wakati unafanya hivyo hakikisha unabana pumzi na kuiachia papo kwa hapo (hakikisha huiachii kwa muda mrefu yani in sec unabana na kuiachia).


Psssssssssssi: Sometimes u have 2 be a little selfish ei? Wanaume wakibana pumzi wanachelewa kufika lakini mwanamke ukibana pumzi unawahi kufika.....hii ni kutokana na uzoefu na nime-share na baadhi ya wanawake na wamefanikiwa kufurahia ngono kama ninavyofurahia mimi.


Karibu sana na kila la kheri ktk jaribio hili

Team Truth (Dinahicious)::::Ni kweli Wanaume wanapenda "Saa sita" Kifuani?


Sina hakika ni kwanini wenzetu (wanaume) wanapenda Matiti wakati sisi (wanauwake) ndio tunao....... ikiwa yatafanyiwa "kazi" vizuri na kwa utaalam. Ukiachilia mbali hilo, matiti hutufanya tuhisi kuwa ni "wanawake" pia ni Mwanzo mzuri wa maisha ya mtoto).


Nakumbuka mara ya kwanza kuvaa Sidiria ilikuwa 2003, sikuwa nahitaji lakini nilidhani kuwa kuvaa Sidilia ndio "uanamke", basi nikaenda kupima size ya Matiti ili kupata "Bra" itakayonitosha vema. Wahudumu wakanishangaa na kusema kuwa ninge-save pesa nyingi kwa kutovaa "Bra" kwani sihitaji, lakini kwa vile nilitaka kujihisi kuwa ni mwanamke nilisisitiza kupata "Bra" yangu ya kwanza....TMI i know, sorry hihihihi....


Katika hali halisi hakuna Mwanaume anaependa kukutana na mwanamke ambae matiti tayari yapo tumboni (inategemea na ukubwa), hiyo haimfanyi mwanaume huyo kuchukia matiti yaliyoanguka ila angependa yaanguke akiwa Mkewe na sababu  iwe ni kunyonyesha watoto wao.


Hebu badilishakibao wewe ndio uwe mwanaume etii....alafu unakutana na na titi zipo tumboni, hapo hajanyonyesha/Zaa, utakuwa hujui raha ya  matiti yaliyosimama na pengine siku moja ungependa kupata uzoefu huo....Hebu fikiri.


Kwa bahati mbaya wanawake wengi kwenye jamii rejea topic ya Jinsi ya kutunza, wengi hujiachia tu kipindi ambacho matiti hayo yanahitaji "support". Hakika Matiti kuanguka ni kutokana na kunyonyesha watoto wa Mumeo, lakini kumbuka kuwa sio Wanawake wote wenye matiti yaliyoanguka wamenyonyesha, Wamezaa, Wametoa mimba au wanawaume/wapenzi....kwamba matiti yao yalianguka kitambo kabla hawajanyonyesha kutokana na kutoyatunza vema.


Ikiwa mumeo alikukuta ukiwa na matiti Saa sita bila shaka ataendelea kuyapenda akijua kuwa wanae waliyatumia "early days of their lives", obviously atakuwa amekubali mabadiliko uyapatayo kutokana na Uzazi....lakini at least aliyakuta Wima na yeye ndio kachangia yatazame Chini (baada ya kunyonyesha watoto).


Ukweli wenye maumivu ni kuwa, Asilimia kubwa ya wanaume wangependa matiti ya wake zao au wapenzi wao yadondoke wakiwa nao na sio wayakute yakiwa hivyo (matiti yamedondoka). Hali inayofanya wengi wao kuzungumzia u-wima wa matiti na kucheka au kubatiza yale yaliyolala kuwa ni Malapa.


Mimi binafsi huwa sipendezwi na hilo na siku zote huwa nasema kabla hujamcheka mwanamke mwenye matiti yaliyolala hakikisha wanawake kwenye familia yako bado matiti yao yapo wima na muhimu kabisa ni je Matiti ya mama yako uliyonyonya bado yamesimama(saa sita)?


Ikiwa kwa bahati mbaya wewe ulichelewa ama ulikuwa hujui namna ya kutunza matiti wakati yananza kujitokeza hakikisha Wanao wa kike wanajua(wafundishe), pia hakikisha unayapa "support" yakutosha unapofanya Mazoezi, Unapo karibia hedhi, unapokuwa Hedhini, utakapo kuwa Mjamzito na wakati unanyonyesha.

CHUPI NA SHANGA ZA MSANII SHILOLE ZAANIKWA NJE- FIESTA



 

UPDATE: MAJAMBAZI YALIYOVAA SARE ZA POLISI YAVAMIA HABIB AFRIICAN BANK NA KUPORA MAMILIONI




Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha.


 Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo..

Habari  zaidi  baadae. 

TRAFFIKI FEKI ALIYEKAMATWA HIVI KARIBUNI ALIKUWA NI MFUNGWA WALIYETOROKA GEREZANI




MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani.

Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.

Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.

“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.

“Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.

“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.

“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.

Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.

Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.

Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:

“Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”

Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.

Tuesday, August 27, 2013

yaliyo jiri jana:::::ACTRESS AUNT EZEKIEL ACHANWA VIBAYA NA CHUPA AKIWA CLUB.

Actress maarufu Swahiliwood Aunt Ezekiel amechimbwa na kitu chenye ncha kali kinachodaiwa kuwa chupa katika mkono wake wa kushoto. Tukio hilo lilitokea juzi katika ukumbi wa Club Billicanas wakati Wema Sepetu akitambulisha wasanii wapya wa Bongofleva. Habari ambazo bado sio rasmi ni kuwa huenda muigizaji huyo alikumbwa na tukio hilo hatari kutokana na issue za kimapenzi yaani kugombea mwanaume siku za nyuma au sasa. Tutakujuza zaidi kinachoendelea. Ugua pole Aunt. Angalia picha chini jinsi actress huyo alivyojeruhiwa.......


http://swahiliworldplanet.blogspot.com/2013/08/actress-aunt-ezekiel-ajerehiwa-vibaya.html (source)
Mkono uliojeruhiwa kabla ya kufungwa
                                                 Baada ya kufungwa







Mama ajifungua watoto wawili walioungana Dar, mmoja hana kichwa

Share  Print

Mkazi wa Zanzibar, Pili Hija akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam jana na watoto wake walioungana.  Picha na Juliana Malondo
Mtoto huyo ambaye hana kichwa anapumua pia akiguswa anapata hisia na kutingisha mguu mmoja.
Dar es Salaam. Mkazi wa Jang’ombe Visiwani Zanzibar, Pili Hija (24), amejifungua watoto walioungana huku mmoja akiwa hana kichwa.
Watoto hao ambao wapo Wodi namba 36 katika Jengo la Wazazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili mbali na kuzaliwa mmoja akiwa hana kichwa, wameungana sehemu ya uti wa mgongo, mkono mmoja na wanatumia njia moja ya haja kubwa.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, mama wa watoto hao, alisema: “Nilijifungulia nyumbani, nilisikia uchungu mara moja na hapo hapo nikajifungua kwa njia ya kawaida na jirani yangu ndiye aliyenisaidia,”alisema na kuongeza:
“Nilijifungua saa moja  asubuhi, nilijua nitazaa pacha kwa kuwa nilishafanya kipimo katika Hospitali ya Makunduchi, wakaniambia nitajifungua pacha lakini mmoja si binadamu ni kiwiliwili.
“Nimeolewa, mume wangu ni mwanajeshi, nina watoto wengine wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume, mume wangu hajui tukio hili kwani yupo kambini Zanzibar na hatuna mawasiliano yoyote kwa sasa,” alisema.
Daktari wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Zaituni Bokhary alisema; “Hii ni mara ya kwanza kwa jambo hili kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Mara ya mwisho lilitokea mwaka 1984.
“Tulikuwa tufanye upasuaji leo lakini tumeahirisha na utafanyika Alhamisi (kesho) asubuhi katika Kitengo cha Mifupa cha Muhimbili (Moi).”
Msimamizi wa Wodi ya Watoto walikolazwa, Dk Edna Majaliwa  alisema: “Hakuna sababu maalumu kitaalamu  inayosababisha watoto kuungana, mara nyingi zinapokutana mbegu za X na Y na kutengeneza mimba kunakuwa na hatua za ukuaji wiki nne, wiki nane, wiki 12, 16 na kuendelea.

KAGAME HATAKANYAGA TENA ARDHI YA TANZANIA.....WABUNGE WA RWANDA WASUSA JIJINI ARUSHA

RAIS Paul Kagame wa Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete.

Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Mwenendo wa hayo yaliyojitokeza jana katika Bunge la Afrika Mashariki hadi kikao kuvunjika, msingi wake ni mgogoro unaowagusa wakuu hao wawili wa dola.

Habari zilizolifikia gazeti hili toka katika vyanzo vyake mbalimbali vilivyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, lakini pia katika vikao vya Bunge hilo la Afrika Mashariki vinavyoendelea jijini Arusha zinaeleza kuwa, Rais Kagame hata kama ataalikwa kuja nchini leo, hatakuja.

MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa jambo hilo tayari limethibitishwa na Wabunge wa Rwanda wanaohudhuria vikao vya (EALA).

Taarifa toka ndani ya Bunge hilo zilizolifikia MTANZANIA Jumatano zinaeleza kuwa, tayari mzimu wa msigano huo uliojitokeza baina ya wakuu hao wawili wa dola, umeanza kuwavuruga wabunge hao baada ya jana kikao cha Bunge hilo kuvunjika, kutokana na kuibuliwa kwa hoja ya kutaka vikao vya Bunge hilo kufanyika kwa utaratibu wa kuzunguka kila nchi.

Zinaeleza zaidi kuwa; Ni katika hoja hiyo wabunge wa Kenya na Rwanda walionekana kuungana na kuwa kitu kimoja na hivyo kususia kikao hicho cha jana, jambo ambalo lilimlazimisha Spika wa Bunge hilo, Magreth Zziwa kuvunja kikao.

HALI ILIVYOKUWA

MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa, wabunge hao walianza kutoka ndani ya kikao kilichokuwa kikiendelea jana, baada ya mmoja wa wabunge hao kutoka Rwanda, James Ndahiro kuomba mwongozo kwa Spika.

Habari zinaeleza kuwa chanzo cha mbunge huyo wa Rwanda kuomba mwongozo, kilitokana na Mbunge kutoka Kenya, Peter Mathuki kutoa hoja ya kutaka suala la vikao hivyo kufanyika kila nchi wanachama, lijadiliwe.

“Sasa baada ya mbunge huyo wa Kenya kutaka suala la vikao vya Bunge kufanyika kila nchi wanachama yaani ‘rotation’ lijadiliwe pale kikaoni, Spika akamwambia hilo ni jambo la haraka sana na ikizingatiwa imebaki wiki moja vikao viishe na kwamba kama anataka lizungumziwe, alilete kama ‘motion’.

“Baada ya Spika kujibu hivyo, ndipo mbunge wa Rwanda akaomba mwongozo kwa Spika…Spika akamjibu kwamba anataka mwongozo gani tena wakati ameshamjibu yule wa Kenya, ndipo wabunge wa Rwanda wakatoka ndani ya kikao wakisema hawataki kuburuzwa huku wakifuatiwa na wa Kenya.”

Taarifa zaidi zilieleza kuwa kitendo hicho ambacho kilisababisha kikao kuvunjika, kilikwamisha kuapishwa kwa Waziri mpya wa EALA kutoka Rwanda.

Ilielezwa kuwa baada ya wabunge hao kutoka, Spika aliahirisha kikao kwa kutumia kanuni kwamba, baada ya dakika 15 warudi.

“Baada ya dakika 15 tuliporudi, wabunge wakawa wachache huku wale wa Rwanda na Kenya hawakurudi tena na waliorudi walikuwa jumla 13 pamoja na Spika kati ya wabunge 45. Ndipo Spika akasema hatuwezi kuendelea na kikao kutokana na uchache wa wabunge, hivyo kikaahirishwa hadi kesho (leo),” kilisema chanzo chetu hicho.

Hata hivyo wakati hayo yanajitokeza, utaratibu wa vikao vya Bunge la Afrika Mashariki  unaelekeza kuwa vitafanyikia Arusha ambako ni makao makuu.

Habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, Kamati ya kuratibu Mambo ya Bunge iliyokutana Entebe Uganda, ilipanga kuwa kwa mwaka vikao vya Bunge vitakuwa sita huku vitatu vikifanyika Arusha ambako ni makao makuu, kimoja Nairobi na vingine viwili bado haijajulikana.

Pamoja na Kamati kufikia uamuzi huo, bado inaelezwa kuwa baadhi ya wabunge wanapinga vikao hivyo kuendelea kufanyika na hasa wa Rwanda ambao inadaiwa kuwa wamepewa maagizo fulani kutoka kwenye Serikali yao

Mbali na hilo la vikao, nyufa nyingine zinazoelezwa kuhatarisha msingi wa Bunge hilo, ni kile kinachodaiwa kuwapo kwa utendaji wa upendeleo wa Spika, Margaret Zziwa.

Kwamba Spika Zziwa amekuwa akishutumiwa kupanga safari za nje kwa upendeleo na kwamba hazieleweki zinapangwaje.

KAGAME KUTOKANYAGA TANZANIA

Wakati hayo yakijiri, imeelezwa kuwa hata Rais Kagame, akialikwa kuhutubia vikao vya Bunge hilo, hataweza kuja nchini kutokana na mgogoro uliopo.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili toka ndani ya bunge la EALA, zinaeleza kuwa wabunge kutoka Rwanda wananung’unika vikao kufanyika Arusha na wameeleza bayana kwamba itakuwa vigumu kwa rais wao kuja hapa nchini endapo ataalikwa na Spika wa Bunge hilo kuja kuhutubia katika vikao hivyo.

“Kwa kawaida vikao vya bunge vinapofanyika, mara nyingi anayehutubia vikao ni Mwenyekiti wa EAC, ambaye kwa sasa ni Yoweri Museveni na rais wa nchi ambako vikao vinafanyika, lakini wakati mwingine spika anaweza akaamua na kumteua rais kutoka nchi yoyote.

“Sasa Spika akimteua Kagame ni dhahiri itakuwa ngumu kuja Tanzania kutokana na mgogoro unaoendelea baina yake na Rais Kikwete,” kilisema chanzo chetu hicho cha habari.

Msigano wa kauli baina ya viongozi hao wakuu wa dola, ulijitokeza baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri kwa Rais Kagame wa kukaa meza moja na waasi wa FDLR.

Hata hivyo baada ya siku chache, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete hadi kufikia kutoa kauli zenye vitisho dhidi yake.

Tangu Rais Kikwete alipotoa ushauri huo, Kagame amekuwa akiendelea kutoa lugha zisizo na staha kwa Tanzania.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda, navyo vimekuwa na mwelekeo huo huo, ambapo hivi karibuni vilianza kuhusisha ushauri huo wa Rais Kikwete kuwa msingi wake unatokana na undugu uliopo kati ya mke wake, Mama Salma Kikwete na wabaya wa Kagame.

Kwamba mke wa Rais Kikwete ni binamu wa kiongozi wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana, habari ambazo zimekanushwa vikali na Serikali.

Ni katika mwenendo huo huo, wiki iliyopita ilibainika kuwa Rwanda na Uganda zinakusudia kutangaza kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao.

Katika hilo, leo Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda pamoja na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajiwa kuzindua Gati ya bandari ya Mombasa yenye thamani ya dola za Marekani milioni 66.7 ambayo ni zaidi ya Sh bilioni 100 za Kitanzania.

Bandari hiyo ambayo itaongeza uwezo kwa asilimia 33, Rais Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya Afrika Mashariki (EAC), ataongoza zoezi hilo la uzinduzi.

Baadhi ya wachambuzi wa sayansi ya kiuchumi, wanasema kuwa endapo Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia bandari ya Dar es Salaam, hizo zitakuwa ni habari mbaya kwa nchi.


 -Mtanzania

Lukuvi: Wabunge wengi wamo orodha ya dawa za kulevya


 Print 

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.
Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.
“Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.
“Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu,” alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.
Katika swali lake ambalo lilisababisha kelele za kuzomea, Natse alitaka majina hayo yatajwe hadharani. Hata hivyo, hali ilitulia baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati na kusema: “Hii tabia ya zomeazomea siitaki humu ndani, acheni tabia hiyo lazima mumsikilize mtu kwa kile anachokisema kwanza lakini mtindo huu si mzuri...”
Patashika hiyo ilitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige aliyetaka kujua iwapo Serikali inaweza kuwaambia Watanzania ukubwa wa biashara hiyo nchini na kama haioni kama kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na mizigo katika viwanja vya ndege na juhudi za Serikali kumaliza tatizo hilo.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo hapa nchini unadhihirishwa na idadi ya Watanzania 274 waliokamatwa kati ya mwaka 2008 hadi Julai mwaka huu kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya katika nchi mbalimbali za nje.
Alisema Serikali inafahamu ukubwa wa tatizo la matumizi ya biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya nchini na alitaja takwimu za ukamataji wa dawa hizo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi Machi, 2012.
Alisema pamoja na kukamatwa kwa Watanzania hao nje ya nchi, wageni 31 wanashikiliwa mahabusu katika Magereza ya Keko na Ukonga, Dar es Salaam ambao ni raia wa Iran, Pakistan, Senegal na Afrika Kusini.
Hata hivyo, katika swali lake la nyongeza, Magige alisema uteketezaji wa dawa zinazotajwa kukamatwa umekuwa wa siri kiasi cha kutiliwa shaka kuwa huenda zinachukuliwa na maofisa waliozikamata ndiyo maana hakuna uwazi.
Kuhusu hilo, Waziri Lukuvi alisema suala la uteketezaji wa dawa hizo hauko wazi kutokana na sheria zilizopo kutotoa nafasi ya kuteketezwa mapema kwa kuwa zinatumika kwa ajili ya ushahidi akisema wakati mwingine hukaa zaidi ya miaka 10.

FOOLISH AGE" YA LULU YAENDELEA KUWA GUMZO NCHINI




Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 

 

Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya kila binadamu katika kila hatua anayopitia katika ukuaji wake.Ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Sauti,Picha hadi maeneo yaliyotumiwa kucheza filamu.Pamoja na kuwepo lulu humo pia utamuona Msanii Mkongwe Jengua.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited na Itakuwa ikisambazwa Na Proin Promotions Limited.Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu.

Monday, August 26, 2013

BALE KUVUNJA REKODI YA CHRISTIAN RONALDO


Real Madrid and Tottenham have agreed a world record €100 million deal for Gareth Bale to join Real Madrid.

Spurs chairman Daniel Levy finally accepted the Spanish giants’ offer on Sunday and official confirmation of the transfer is expected to be made imminently.
ALL SET FOR MADRID
Alberto Pinero | Goal Spain
Bale isn't officially a Real Madrid player yet - but you wouldn't have thought that by the way he is being paraded in Madrid. He is all over the sports newspapers, radio stations and TV sports news channels. And let's not forget he's been the talk of the Real Madrid, and even Barcelona, press conferences.

It has been this way for several weeks now. Even at the Santiago Bernabeu as early as last Thursday there were people wearing the Madrid shirt with 'Bale 11' emblazoned on the back.

The clubs have come to an agreement on a straight cash deal to be paid in three installments, as Bale becomes the most expensive player in history, eclipsing the €93m Madrid paid Manchester United for Cristiano Ronaldo in 2009.

Tottenham have spoken to Madrid at length about including players in the deal, but left-back Fabio Coentrao is not part of the agreement while Real refused to include young striker Alvaro Morata in the transfer.

Bale is expected to sign a six-year contract at the Santiago Bernabeu reported to be worth €10m a year after tax, where pictures emerged on Friday of the club setting up a stage inside the stadium for his presentation to the supporters.

Tottenham’s decision to accept Real’s offer brings to an end a protracted summer of speculation and negotiations over the Welshman’s future.

Bale shocked Spurs when he told the club he wanted to leave during their pre-season tour of Hong Kong in July while Real Madrid were very public in their courtship of last season’s PFA Player of the Year.

Perez was desperate to make Bale his latest galactico signing after missing out to Barcelona in the race for Brazilian star Neymar at the start of the summer.

Bale has spent the weekend in Marbella in Spain having been given two days off by Villas-Boas, and he is expected to return to England briefly on Monday before flying out to Madrid.

Tottenham are hoping to conclude a €35m move for Roma winger Erik Lamela in the next 48 hours, with the Argentine considered a direct replacement for Bale, who was pencilled in to play on the right of a front three this season.

Spurs have agreed the basics of the deal but remain cautious following Willian’s decision to join Chelsea from Anzhi Makhachkala despite completing a medical and agreeing terms with the north Londoners.

Romanian centre-back Vlad Chiriches is also expected to join from Steaua Bucharest this week in a €9.3m deal, while manager Andre Villas-Boas still wants a left-back and a creative player before the transfer window closes on September 2.

Sunday, August 25, 2013

NICK MBISHI ATANGAZA RASIMI KUWA YEYE NI MUATHIRIKA WA UKIMWI


Tumekuwa  tukishuhudiwa  vituko  mbalimbali  vya  wasanii wetu  ambao  wamekuwa  wakihangaika  usiku  na  mchana  kuusaka  umaarufu....

Wapo  ambao  wamekuwa  wakivua  nguo  zao  jukwaani, wapo  ambao  wamekuwa  wakipiga  picha  za  uchi  na  kuzitupia  mitandaoni.Yote  hiyo  ni  kutafuta  Jina  au  umaarufu ambao  mimi  binafsi  nauita  ni  umaarufu  wa  kishamba.....

Leo  Nick  Mbishi  ametoa  kituko  ambacho  kimenifanya  niamini  kuwa  wasanii  wetu  wana njia  mpya  kwa  sasa  za  kutaka kujulikana ( kuwa  maarufu).

Katika  account  yake  ya  Twitter, Nick  Mbishi  alitoa  post  moja  ikielezea  kuwa  yeye  ni  muathirika  wa  ukimwi.

Post  hiyo  ilikuwa  na  taswira  mbili  za mafumbo . Fumbo  la  kwanza  linamaanisha  kuwa  Yeye  NI  mwathirika  wa  UKIMWI  huku  fumbo  la  pili  likimaanisha  kinyume  chacke.

Baada  ya  post  hiyo, mijadala  kadhaa  ya  watu iliibuka  kwenye  mitanado  ya  jamii.Wapo waliompa  pole  na  wapo  waliompongeza  kwa  ujasiri  wake...

Cha  kushangaza  ni  kwamba, baada  ya  Nick  kuona kuwa issue  imekuwa  serious  kuhusu  madai  ya  yeye  kuwa  na  UKIMWI, alirudi  tena  Twitter  na  kuanza  kuilaumu  mitandao  ya  kijamii....

Kinachonishangaza  ni  kwamba, Nick  anakaumu  nini  wakati  alitamka  mwenyewe??.Hizo  ni  sifa  za  kishamba  za  kutaka  jamii  ikuongelee  na  kukujadili...

Kama  umeamua  kujitangaza, basi  kuwa  serious  ili  watu  wajue  moja.

Hii   ndo  post  yake.

http://freebongo.blogspot.com/2013/08/nick-mbishi-atangaza-rasimi-kuwa-yeye.html