Tuesday, August 27, 2013

FOOLISH AGE" YA LULU YAENDELEA KUWA GUMZO NCHINI




Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 

 

Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya kila binadamu katika kila hatua anayopitia katika ukuaji wake.Ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Sauti,Picha hadi maeneo yaliyotumiwa kucheza filamu.Pamoja na kuwepo lulu humo pia utamuona Msanii Mkongwe Jengua.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited na Itakuwa ikisambazwa Na Proin Promotions Limited.Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu.

No comments:

Post a Comment