Msanii Tundaman amejikuta
akiambulia aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani
akiwakwepa askari polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa
lengo la kumkamata....
Chanzo cha Tunda man kusakwa na polisi ni deni la sh. laki
nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mwanadada mmoja (
jina kapuni)....
Taarifa zinadai kwamba, baada ya kupewa hela hiyo, Tunda man
aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa mrembo huyo. Kila
akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi ya
nguoni.....
Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo aliamua kulifikisha swala
lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa mikononi mwa
polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni lake
kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013
Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza kulipa kiasi chochote na
wala hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyomfanya mwanadada huyo
arudi kuripoti polisi....
Polisi walianza jitihada za kumsaka ambapo leo majira ya saa
nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana ) kwa lengo la
kumkamata.....
Bahati nzuri au mbaya, Tundaman alifanikiwa kuwatoroka polisi
akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa mashuhuda) na kutokomea
kusikojulikana...
Ifuatayo ni HATI YA MAKUBALIANO yao ambayo mpekuzi wetu amefanikiwa kuipata....
Kama
kuna jambo ambalo linaichafua Tanzania katika jukwaa la kimataifa kwa
siku hizi, basi ni tatizo la usafirishaji wa dawa za kulevya.
Zamani tatizo hili halikuwa kubwa sana, ni mtanzania mmoja mmoja sana
alikuwa akikamatwa nje kwa kusafirisha dawa za kulevya. Kwa hiyo jina la
nchi yetu lilikuwa linasikika mara moja moja sana au kwa bahati mbaya
kuhusiana na tatizo la dawa za kulevya. Lakini katika siku za hivi
karibuni tumesikia kuwa kuna watanzania wanakamatwa Ulaya, Amerika
Kaskazini, Amerika Kusini, Asia na hata katika nchi za Afrika, kama
ilivyotokea majuzi huko Afrika Kusini. Kwa sasa ukisikia jina la
Tanzania linatajwa kuhusiana na tatizo la dawa za kulevya, si bahati
mbaya tena na si mara moja moja kama zamani.
Serikali yetu imekuwa ikijitahidi sana kujenga jina zuri la Tanzania na
kuitanganza Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani, nchi yenye vivutio vingi
vya utalii na yenye ukarimu kwa wageni. Na kweli kama ukitembelea nchi
yoyote yenye watu wanaoifahamu Tanzania, si vigumu kusikia Tanzania
ikisifiwa, lakini kama ukiona mtu amekaa kimya, basi ujue kuna uwezekano
kuwa hataki kutaja suala la dawa za kulevya.
Mwanzoni nilikuwa naamini kuwa watanzania ni watu wenye maadili ambao
wanapokwenda nje ya nchi wanakumbuka kuwa “mabalozi wazuri” wa nchi.
Lakini baada ya kutembelea sehemu mbalimbali duniani, hasa nchi za Asia
na Asia Kusini Mashariki, na kukutana na wenyeji na kuwauliuza mtazamo
wao kuhusu Tanzania na watanzania, nikagundua kuwa sifa zote nzuri za
Tanzania zinafunikwa na sifa mbaya moja au mbili. Kubwa ni tatizo la
dawa za kulevya, na nyingine ni ukahaba (Hong Kong).
Pamoja na kuwa ni watanzania wachache sana wanaosafirisha dawa za
kulevya, ni hao wachache ndio wanaofanya jina la watanzania wengine
walio wengi lichafuke, na kuwafanya watanzania wanaokwenda nje ya
Tanzania kwa malengo halali, kama vile biashara, michezo na hata utalii,
wakumbwe na matatizo wasiyostahili.
Zamani nilikuwa ninakasirika sana ninapotolewa kwenye mstari wa uwanja
wa ndege na kuanza kupekuliwa na kuulizwa maswali ‘ya kipuuzi’, kana
kwamba mimi ni mhalifu au mtuhumiwa wa uhalifu. Nilikuwa najihisi kuwa
mimi ni mhanga wa ubaguzi wa rangi, kitu ambacho sikutegemea kutoka kwa
nchi marafiki zetu. Kuna wakati hata nilifikia hatua ya kukwaruzana na
maofisa wa uwanja wa ndege, kwa kuona wananitendea isivyostahili. Lakini
baadaye baada ya kuangalia hali halisi na kuona matendo yanayofanywa na
baadhi ya watanzania wanaokuwa nje ya Tanzania, nikagundua kuwa
wasiwasi walionao maofisa wa viwanja vya ndege vya nchi za Asia kuhusu
watu wenye pasi za kusafiria za Tanzania, ni wa haki na unaeleweka, si
ubaguzi wa rangi na si ubaguzi dhidi ya watanzania. Kama ni ubaguzi wa
rangi, basi matendo ya baadhi yetu ndio yanawapa kisingizio cha kufanya
hivyo.
Kinachonifanya nisione kuwa ni ubaguzi wa rangi ni kuwa, nchini China
kwa mfano kuna adhabu kali sana kwa watu wanaokamatwa kwa makosa ya dawa
za kulevya, wachina wengi wamehukumiwa adhabu ya kifo.
Lakini cha ajabu ni kuwa watanzania wanaokamatwa kwa makosa sawasawa na
wanayofanya wachina, wanapewa vifungo virefu na adhabu ya kifo, lakini
hadi sasa hakuna mtanzania aliyenyongwa ikilinganishwa na wachina na
wafungwa wa mataifa mengine.
Kumekuwa na habari za kupotosha kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya
Tanzania kuhusu jambo hili, lakini ukweli ni kuwa Mpaka sasa hakuna
mtanzania aliyehukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya dawa za kulevya na
adhabu yake kutekelezwa. Ni vigumu kujua ni kwanini China haijawanyonga
watanzania, lakini ukiangalia sababu ya wachina kutowachukulia hatua
kali watanzania, utaona kuwa wanathamini sana urafiki uliojengwa na
viongozi wetu, hasa mwalimu Nyerere na mzee Salim Ahmed Salim. Kwa hiyo
ukiona jinsi wenyeji wanavyochukuliwa hatua kali, na sisi watanzania
“kudekezwa”, hata ukikutana na vitendo vinavyokukosesha raha unapopita
uwanja wa ndege, basi inabidi uwe mpole mara moja.
Pamoja na kuwa kila suala la dawa za kulevya linapotajwa, utakachoona
kwenye vyombo vya habari ni kuwa kuna mtandao mkubwa wa siri, lakini ni
kama tunapuuza madhara yanayoletwa na jambo hili kwa uhusiano kati ya
nchi yetu na nchi nyingine, na usumbufu linaoleta kwa watanzania wengine
wasio wasafirishaji wa dawa za kulevya.
Inasikitisha kuona kuwa kati ya watu kutoka nchi za Afrika Mashariki,
ni watanzania ndio wanaokamatwa zaidi na dawa za kulevya kuliko wale
wakenya na waganda. Na hata watanzania wanaokamatwa, wengi wanatoka
katika Mikoa miwili ya pwani, ambako baadhi ya vijana wanaona ni “ujiko”
kusafirisha dawa za kulevya. Ukiongea na vijana hao, unaweza kuona kuwa
hawana elimu hata kidogo, kwani hata uwezo wao wa kuandika kwa
Kiswahili na uwezo wa kuongea Kiswahili na kujenga hoja ni mdogo sana,
ndio maana inaonekana ni rahisi kwao kurubuniwa kuliko vijana wa Kenya,
Uganda na wa nchi nyingine za Afrika Mashariki. Wengi wao wanasema wanaahidiwa kati ya dola elfu mbili na elfu nne wakifikisha “mzigo” salama.
Kwa kweli hizo si pesa nyingi ikilinganishwa na hatari ya kazi yenyewe,
na hasa ukizingatia kuwa kwa mtanzania anayejituma kufanya kazi
nyumbani, anaweza kupata pesa hizo.
Kwa hapa China, mpaka sasa naweza kusema kwa sasa tatizo limefikia
kiwango cha kutia hofu, na hasa kwa Hong Kong na Makau ambako kuna wafungwa zaidi ya 100 wa kitanzania. Tofauti na siku za nyuma, idadi ya wafungwa wa kike inazidi kuongezeka siku hadi siku ambapo kwa sasa kuna wafungwa wa kike zaidi ya 20
katika magereza ya China bara na Hong Kong. Kutokana na hali hiyo nina
wasiwasi kuwa huenda ile hadhi ya watanzania kuingia katika miji hiyo
bila Visa huenda iko mashakani. Lakini vigumu kwangu kama mwandishi wa
habari kujua undani wa tatizo hili. Ninachojua ni kuwa kuna watanzania
wengi wako gerezani, kutokana na kukamatwa kwa makosa yanayohusiana na
dawa za kulevya.
Niliwahi kumuuliza aliyekuwa balozi wa Tanzania hapa China na balozi wa
sasa kuhusu athari ya tatizo hili kwenye uhusiano wa kidiplomasia kati
ya China na Tanzania, wote walioonesha kukasirishwa na kusikitishwa na
jambo hilo, na kusema linatia aibu. Lakini mabalozi hao hawajui ni nani
anayewatuma watanzania wanaokamatwa na dawa za kulevya. Waliokamatwa nao
hata siku moja hawataji ni nani aliyewatuma, wao ni kama watu waliokula
yamini ya kutosema lolote, hata kama wanapewa adhabu ya kifo. Hata
hivyo, wafungwa wanaeleza tu kwamba “Kuna mtandao mkubwa ambao unahitaji
ushirikiano mkubwa kupambana nao, zinakopelekwa na zinakotoka dawa
hizo”.
Hivi karibuni tumesikia alichokifanya Dk Mwakyembe kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, yeye anaona kuwa uwanja unaobeba
jina la Mwalimu Nyerere haupaswi kuhusishwa na dawa za kulevya.
Alichofanya Dk Mwakyembe pale uwanja wa ndege kwa kweli ni jambo zuri,
na kama asingefanya hivyo huenda watanzania tungeendelea kuwa kizani
kuhusiana na mambo yanayoweza kuwa yanaendelea katika forodha zetu.
Lakini tukiangalia kwa undani tunaweza kuona kuwa, kama uhalifu huo
unatokea kwenye uwanja wa ndege unaotakiwa kuwa na usalama mkali, hali
ikoje kwenye forodha nyingine mbali na ile ya uwanja wa ndege wa mwalimu
Nyerere ambako hakuna kamera za video, ambako Dk Mwakyembe hawezi
kwenda kwa ghafla? Kuna Namanga, Holili, Horohoro, Silari, Tunduma nk,
hali ya huko ikoje? Dk Mwakyembe anatakiwa kuhakikisha kuwa
kilichofanyika katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kifanyike
katika forodha zote. Dk Mwakyembe analia na jina la Mwalimu Nyerere,
lakini ni vizuri watanzania wote tukikumbuka kuwa tunatakiwa kulia na
jina la nchi yetu, Tanzania.
Kama hali hii ikiendelea inaweza kufika hatua kuwa wanafunzi,
wafanyabiashara, wanamichezo, wagonjwa na hata watalii kutoka Tanzania
wanaokwenda nje ya nchi, wote watawekwa kwenye kundi la washukiwa wa
biashara ya dawa za kulevya.
- See more at:
http://www.fikrapevu.com/watanzania-zaidi-ya-100-wako-gerezani-nchini-china-kuhusiana-na-dawa-za-kulevya-20-ni-wanawake/#sthash.WFUZxGSe.dpuf