Ndoa yoyote ambayo mke au mume hafiki kilele hiki cha Mlima Kilimanjaro…,hiyo siyo ndoa inayokwenda sawa na kuna madhara makubwa kwa pande zote, kwa maana ya mwingine kuweza kuamua kutoka.
Ni vizuri walio kwenye ndoa kujifunza namna ya
kupeana raha iwapasayo wanandoa kuipata. Kama unafikiri mkeo unaye kwa
sababu amekuja kutafuta kula au kununuliwa magari na nguo, hilo ni kosa.
Tafakari namna ya kupeana raha kwa kila kona.
Kama ni kula, kila mtu anaweza kujitafutia kwa njia mbalimbali kama ni kuuza mama ntilie na kadhalika.
Mwanamke yuko kwa mume kwa sababu anahitaji kupata
vitu ambavyo wanawake huvipata kutoka kwa wanaume; …Mume ndiyo kichwa,
iongoze ndoa yako vizuri kwa hekima; …Kichwa kikiwa ‘bangi’, ubavu (mke)
atafanya nini?
Ni suala la lazima
Kwa asili, inatakiwa mke na mume kufanikisha zoezi
hilo la kuwezeshana kufika kileleni na ni jambo muhimu kama ilivyo kutoka
jasho mwilini, maana siyo tu mwili unaondoa uchafu ndani ya mwili, pia
inasaidia kuupoza mwili kuwa sawasawa.
Najua wapo wanaoweza kusema aaah mbona mimi nimekaa mwaka sitaki tena mwanaume au mwanamke na sijapata madhara… Inawezekana ni kweli, lakini wengi hupata madhara.
Kadhalika kuna wengine wanafanya vitu vya hatari
kama kutumia vitu mbalimbali kama mwanasesele (sex toys) au mashine
maalumu zenye umbo kama la mwanaume au wengine kujichua au kusagana.
Ukidumu bila tendo la ndoa muda mrefu, baadhi ya
madhara madogomadogo ni kama kuwa na hasira za mara kwa mara katika
mambo madogo, hii hasa kwa wanawake ambao walishawahi kuwa na uhusiano
unaokaribiana kuoana au waliwahi kuwa kwenye ndoa kisha wakatoka.
Kwa wanaume madhara yake ni kupendelea zaidi
kuangalia picha za ngono. Kwa wote kwa maana ya wanaume na wanawake huwa
na hali ya kusahausahau.
Kwa wanawake, wapo ambao hutokwa damu nyingi
wakati wa hedhi. Kwa watu wote yaani wanawake na wanaume hupenda kurukia
mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu) na
wakati mwingine huongea kwa sauti ya juu hasa kunapotokea migogoro.
Wengine wana uwezo mkubwa wa kutukana au kutoa kauli yoyote unapomuuzi, anasema Leonard Trelawny katika jarida lake la mageuzi alilochapisha, New York Marekani.
Wengine wana uwezo mkubwa wa kutukana au kutoa kauli yoyote unapomuuzi, anasema Leonard Trelawny katika jarida lake la mageuzi alilochapisha, New York Marekani.
Athari nyingine ni kuumwa na kichwa kwa wanaume na wanawake, kupoteza umakini katika kazi na kwa jumla sehemu za kazi wengi wa watu ambao wamesema hawataki tena kusikia mapenzi, siyo viongozi wazuri, wana kauli chafu, hata uamuzi wao mara nyingi siyo mzuri, ingawa siyo wote.
Hali kadhalika siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila
kinga utaambukizwa kirahisi mno. Aidha, unawaweza kuanzisha tabia
nyingine mbaya kama ulevi, kukaa ofisini tu bila sababu.
Dismas Lyassa ni mtaalamu wa uhusiano aliyesajiliwa na Serikali kupitia taasisi ya Global Source Watch
-Mwananchi
-Mwananchi