Saturday, August 3, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU : SABABU KUU ZA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA / MAPENZI (KUJAMIIAANA)

Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano wa mwanamke na mpendwa wake. Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana sana kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.
Visababishi vya tatizo hili kwa wanawake ni;

  • KUSAGANA AU MAPENZI YA JINSIA MOJA KWA WANAWAKE.

  • Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili linaweza kutokea kutokana na msongo wa mawazo ambapo huchangiwa na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa uaminifu katika uhusiano {infedility} nk) na magonjwa mbalimbali.
  • Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au ndoa
  • Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana kwa kuingiliana na ufanyaji kazi wa homoni/kichocheo chengine kinachojulikana kama dopamine (ambayo ndio humfanya mtu kufikia kilele wakati wa kujamiana). Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu nyengine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo (anterior pitituary tumors). Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume(impotence).
  • Kupungua mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
  • Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
  • Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu
  • Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote hupunguza hamu ya kujamiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.
  • Ugonjwa wa kisukari
  • Uvutaji sigara
  • Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
  • Uzito uliopitiliza (obesity)
  • Ugonjwa wa mifupa (arthritis)
  • Utumiaji madawa ya kulevya
  • Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve damage) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
  • Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu,antidepressant medication, dawa za saratani nK.
  • Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo kusababisha uchovu.
  • Ugonjwa wa moyo
  • Saratani ya aina yoyote ile
  • Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression nk.
  • Historia ya kubakwa, au kupata maumivu wakati wa kujamiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari kujamiana au kutotayarishwa vyema kabla ya kujamiana au magonjwa ya zinaa.
  • Tatizo la vaginismus – Hii ni tatizo ambalo husababisha tupu ya mwanamke kuwa ndogo wakati wa kujamiana na hivyo husababisha mwanamke kupata maumivu wakati wa kujamiana.
  • Kupenda intaneti kupita kiasi (addiction) – Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchat au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababishwa msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.
Ni kundi gani la wanawake lililo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili?
  • Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
  • Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
  • Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (menopause- miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri nadepression.

Friday, August 2, 2013

18+ NDANI YA DARASA HURU: MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO




ATHARI za PUNYETO
Wanaume waliowengi hukidhi haja zao kwa kutuliza matamanio yao kwa njia ya kujichua/ kupiga punyeto bila kufahamu madhara yake: Nikweli punyeto inasaidia kupunguza hamu ya tendo na ni njia nzuri ya kujiepusha na zinaa kwa kujilinda na maradhi ila kiukweli ina madhara na madhara yake mara nyingi hutokea kwa mtu anaependelea sana kupiga punyeto, kutokana na utafiti uliofanywa kisayansi imeonekana punyeto ni nzuri kiafya ila endapo kama utakuwa unapiga mara moja moja na sio kila siku. Napenda kuwashauri watu wanaopiga punyeto wawe makini na wasiendekeze jambo hili kwani madhara yake ni makubwa sana na Athari zake kubwa ni hizi zifuatazo:

1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME:
Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inaregea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umeregea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO:
Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya mapenzi na mpenzi wake na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mpenzi wake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kusex.

Athari nyingine ni kama zifuatazo 

3.Uchovu wakati wote 
4.Maumivu ya nyonga 
5.Kusinyaa kwa Nywele/Nywele kunyonyoka 
6.Maumivu ya kende 
7.Maumivu ya kiuno 

Mpendwa wa safu hii hizo ni athari kuu 2 tu, ingawa ziko nyingi ila hizi nilizozitaja ni kwa uchache na ndio zinazo wakumba wanaume walio wengi. Ushauri wangu mimi kama wewe unapiga punyeto basi jitahidi usiwe unapiga kila siku atlist kwa wiki mbili mara moja endapo kama utajisikia hamu ya kusex kama huna mpenzi au ukishindwa acha kabisa.

Thursday, August 1, 2013

SOMA NI MUHIMU SANA SANA NA INASIKITISHA: KANSA YA NGOZI YAMHARIBU MTOTO WA MIAKA 7 VIBAYA SANA....

MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.




“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.

“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi. 

REFERENCE

JOINT MPYA: OMMY DIMPOZ ft J MARTIN - TUPOGO DOWNLOAD IT HERE

DOWLOAD IT HERE

NU JOINT: NEY WA MITEGO ft NEYBA - SALAMU ZAO............. DOWNLOAD

DOWLOAD HAPA

Wednesday, July 31, 2013

KUELEKEA UCHAGUZI 2015: SHEIKH PONDA ISSA PONDA APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS





Ikiwa  imebakia  miaka  miwili  kabla  ya  kufanyika  kwa  uchaguzi  mkuu wa  Rais  na  wabunge  hapa  nchini,baadhi  ya  waumini  wa  kiislamu  wameanza  kupendekeza  wagombea  wa  urais  wanaoona  kuwa wanafaa  ambapo  jina  la Sheikh  Ponda Issa Ponda  limeongoza....

Mapendekezo  hayo  yamedhihirika   katika  mihadhara kadhaa  anayoifanya Ponda  katika  mikoa  mbalimbali  nchini,ambako  amekuwa  akipendekezwa  na  kushauriwa  na  waumini  agombee  nafasi hiyo.....

Walianza  waumini  wa  msikiti  mkuu  wa  Ijumaa  wa  Arusha  alipokuwa  kwenye  ziara  mkoani  humo  ambapo  muumini  mmoja  alisimama  na  kusema  kwamba  kwa  mawazo  yake  anaona  Ponda  anafaa  kugombea  nafasi  ya  urais  kwa  vile  anaamini  kuwa  uwezo  wa   kuongoza  anao..

Alisema  mbali  na  uwezo pia  yuko  makini  katika  kusimamia  jambo lolote  lenya  maslahi  kwa  waislam  na  kwamba  mtu  wa  namna  hiyo  atafanya  vyema  zaidi  akipewa  dhamana  ya  kuongoza  nchi....

Inaelezwa  kuwa Ponda  alipotembelea  Zanzibar  alipata  wakati  mgumu  wa  kuwakataa  waislam  waliojitokeza   kumlaki  katika  misikiti  ya  Mpendae na  Mbuyuni  ambako  alifanya  mihadhara  na  kupendekezwa kugombea  urais  kwa  kura  nyingi  na  waumini  ....

Kufuatia  kusikika  kwa  mapendekezo  hayo,Kisiwa  lilimtafuta  Ponda  ili  kusikia  maoni  yake  juu  ya  maombi  ya  waislam  kumtaka  agombee  urais.

"Sikuwa  na  fikra  hiyo  hata  mara  moja,lakini  maadam limeletwa  nami  ni  kiongozi  wa  taasisi  ninawashukuru  waliofikiria  hivyo...

"Kwa  sasa  siwezi  kuzungumza  lolote  kuhusu  hilo, ntalifikisha  katika  taasisi  na  maulana  ndio  watakaolitazama  na  kutoa  uamuzi." Alisema  Sheikh Ponda

Ponda  alisema  kuwa  inawezekana  waumini  wakawa  na  mtazamo  huo  lakini  viongozi  wakawa  na  mtazamo  tofauti  kabisa,hivyo  akawataka  waumini  kuwa  na   subira  katika  hilo.


REFERENCE

DOWLOAD NEW AND BRAND HIT........... MAKOMANDO - KIBABAA


DOWNLOAD HAPA

SIKILIZA NA DOWNLOAD NEW HIT.... COUNTRY WIZ ft G- NAKO - WATCH ME MASTERING

INGIA HAPA KUDOWNLOAD

NEW MUSIC: DOWNLOAD..... ADAM MCHOMVU - AU SIO

INGIA HAPA KUDOWLOAD

Tuesday, July 30, 2013

SOMA MUHIMU SANA.............BIDHAA 48 HAZITAKIWI SOKONI TBS IMETHIBITISHA.




Shirika la Viwango (TBS) limetangaza orodha ya bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena.

Hatua hiyo ya TBS inatokana na watengenezaji wa bidhaa hizo ambazo awali zilithibitishwa na TBS na kuruhusiwa kutumia nembo yao hiyo ya ubora kumalizika na wahusika kushindwa kuwasiliana na shirika hilo kwa ajili ya uhakiki wa bidhaa zao hizo.

Ofisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.

Bidhaa ziliazoainisha katika tangazo hilo ni pamoja na 
majina ya watengenezaji /wasambazaji katika mabano ni pamoja na karatasi laini ‘tissue’ za Alawi Supplies ya Zanzibar, Milk Marie Biscut za Britania, Maji ya Great Zone, Mishipi na nyavu za kuvulia samaki za Imara Fishnet, maji ya Raha na fulana za Kibo Trade.


Bidhaa zingine ni matofali ya GM Gross, taulo za watoto za Hengan Sanitary, baadhi ya rangi za Chui, beteri za Dry Cell, magodoro ya Jumbo foam, sabuni za Mbasira Investment ya Shinyanga, mifuko ya plastiki ya Centaza na mafuta ya kupikia ya Sun Flower Seed (Sun Shine) na korosho zinazosambazwa na Frabho Enterprises.

Pia taulo za wanawake za Sythentic Detergent (ARIEAL) za Procter&Gambler, mifuko ya B-Twill Jute na A-Twill, mifuko ya plastiki ya Tropical, mafuta ya kupikia ya Sun Flower ya A TO Z Oil Mills, Korosho za Munawar ya Mbeya, Sabuni za kunawia za Brite Chemicals, pipi, lawalawa, mipira ya kutafuna ya rangi mbili.

Vilainisha vya injini (Saud Oil) za Star Composed, betri za 777 kutoka China, maji ya kunywa ya Shia yanayotengenezwa na Siha Beverage, mtindi wa Morani Dairy ya Tanga, pikipiki za Star Shineray, vigae vya Mbezi, sabuni ya Liquid Detergent, mbao zilizotiwa dawa za Mombo, Jam iliyochanganywa ya Les Group ya Musoma.

Orodha hiyo pia inataja Jusi za nanasi za Unnat Fountain ya Morogoro, Maji Uluguru, springi za magari za kampuni ya TASIA, Gypsum zinazotengenezwa na Tanzania Gypsum ya Dar es Salaam, Maji ya Uzima, magodoro ya Plyfoam,Mvinyo wa nanasi wa Kivumbui ya Arusha na mabati ya RD Roofing & Wire Product.

Bidhaa zingine ni unga wa sembe wa Kweniml ya Machame Kilimanjaro, boriti za Ravji Manufacturing, mafuta ya breki za magari ya Automotive Packed ya Dar es Salaam, maJi ya kunywa ya AAMFA, pikipiki za Foshan Fost za China na mvinyo wa matunda wa Victoria Food Product ya Mara pia Jibini, mtindi na maziwa ya Kyaka Milk Processing , Sabuni za kufulia za Jamii za Kampuni ya Mbasira ya Shinyanga.

SIKILIZA NA DOWNLOAD:.. WISE ONE ft JACO BEATS - MALAIKA (PEREMENDE MUSIC EMPIRE)

Produced by JACO BEATS, PEREMENDEE MUSIC EMPIRE BADO WANAENDELEZA UBABE KANDA YA KATI NA HII NI NGOMA YAO MPYA.


BOFYA  HAPA KUDOWNLOAD

PEREMENDE MUSIC EMPIRE DROPS NEW VIDEO:.....WISE ONE ft JACCO BEATS - MALAIKA (OFFICIAL VIDEO)


WATCH AND DOWNLOAD IT HERE

SIKILIZA NA DOWNLOAD SNURA - NIMEVURUGWA




BOFYA HAPA KUDOWNLOAD

DOWNLOAD NEW MUSIC.... JOH MAKIN ft NIKKI wa PILI - BEI YA MKAA.


ILI KUDOWNLOAD BOFYA  hapa

WHY ALWAYS CLOUDS FM!!!!!!!!...."SINA MPANGO WA KUAJIRIWA NA "K....MA" YOYOTE.... (MWISHO MWAMPAMBA)



HALI SI SHWARI KATI YA KITUO CHA MATANGAZO CHA CLOUDS FM NA MWISHO MWAMPAMBA.........

 Mwisho Mwampamba amegeuka  mbogo  na  kufurumua  matusi  ya  nguoni  kwa  Clous Fm  baada  ya  kituo  hicho  kuanza  kumjadili  na  kumchambua...

Mwampamba, ambaye  ni  staa  namba  mbili  wa  shindano  la  big  brother  mwaka  2003  anadai  kutoridhishwa  na  kitendo  cha  Cloud  fm kuanza  kumjadili...

Staa  huyo  amedai  kwamba  yeye  anamaisha  yake  na  hivyo  haoni  haya  ya  kuanza  kufuatiliwa  kwa  kuwa  hana  mpango  wa  kuomba  ajira  kwa  yeyote...

"Clouds fm siwaelewi mnatafuta nini . Nahisi mnatafuta kupakazwa mafuta ya ubuyu . Tafadhali kusaga naona heshima inapungua . 


"Had mifugo yako hujawalea vizuri . Mimi sio msanii na pia sita ajiriwa na k**ma wowote yule . Stay away from me n my family.Ameandika  staa  huyo  katika    account  yake  ya  facebook


SIKILIZA NA DOWNLOAD NGOMA HII:...... A-TOWN HAITAWALIKI- KAPUKU DIGITAL

Ukipata nafasi ya kusikiliza nyimbo hii utagundua kitu kutoka arusha ndani yake yameongelewa mengi sikiliza mwenyewe............




BOFYA HAPA KUDOWNLOAD

MAJINA YA WAUZA UNGA (madawa ya kulevya) HADHARANI : IMEANDIKWA NA WAFUNGWA HONG KONG WENYE ASILI YA KITANZANIA.


CLICK PAGE UNAYO ITAKA KUVIEW VIZURI








SOURCE HAPA

Monday, July 29, 2013

TEAM TRUTH TUNAOMBA RADHI KWA POSTI ILIYOPITA "KUHUSU KUAPDATE ACCAUNT YA MIKOPO'

Tunaomba radhi kwa posti ya kuapdate mikopo iliyo tolewa leo...................... upotoshaji huo umefanywa na moja ya team member wetu baada kusikia habari hizo tangu asubuhi kama ADMIN wa team truth naomba radhi na nachukua nafasi hii kusema kwa wanotakiwa kuapdate na wale tu ambao hawakupata nafasi tya kuupdate mwanzo account zao mwanzo................... POSTI HIYO KWA SASA HAIPO.

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA NA KEEP IN TOUCH

DOWNLOAD NA SIKILIZA NGOMA MPYA YOUNG DEE - KIJUKUU


INGIA HAPA KUDOWNLOAD

TANGAZO KWA UMMA: HIGHER EDUCATION STUDENTS' LOAN BOARD


TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawatangazia waombaji wote wa mikopo wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo kuwa mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ni tarehe 31 Julai, 2013 na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawasisitizia waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: www.olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti:www.heslb.go.tz kabla ya tarehe 31 Julai, 2013.
Kila mwombaji anakumbushwa kusoma kwa umakini mwongozo wa ujazaji wa fomu ya maombi ya mikopo kwa mwaka 2013/2014 na kulipia ada ya shilingi 30,000/= kwa waombaji wapya kwa njia ya M-Pesa.

Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU