Thursday, September 5, 2013

MMHHHH Shoga lafumaniwa na mkewe "likiliwa jicho" ( likiliwa tigo)




Kuna kitu ningependa niwashirikisha marafiki wa ukurasa huu ingawa ni aibu lakini ni vyema pia na akina dada wenzangu na hata vijana wa kiume wajifunze kutoka kwangu.

Mimi ni binti wa miaka 30 na nimebahatika kupata watoto wawili wakiume na wakike na namshukuru muumba kwani wana afya tele.

Niliolewa miaka 5 iliyopita na kijana mmoja ambaye tulikuwa wapenzi kwa takribani miaka sita na baadae tukaona ni vyema tuoane.

Katika maisha yetu ni kweli baba watoto amekuwa mtu asiye na makuu na mwenye kujali na mara nyingi tumekuwa hatuna matatizo madogo madogo kwani yeye ni mzee wa mesheni town.

Nianza kusikia mtaani kuwa mme wangu sio riziki lakini nilipuuzia kwani siku hizi kijana akiwa na maendeleo kidogo na ni handsome basi watu hawataacha kumpa kashfa kibao na hasa ukizingatia kazi za mishemishe nazo huwa na majanga yake.

Hata nilipoambiwa kuwa kwa nini anakuwa karibu sana na waarabu nilipuuza kwani mimi nilimwamini sana mme wangu. Na pia nilijiuliza mbona deal zake nyingi ni dubai na oman kwa hiyo ni kawaida tu ukizingatia huko ndio kuna watu wa rangi hiyo.

Kuna wakati nakumbuka niliwahi kumuomba ruhusa niende kijijini kwetu nikawasalimie wazazi na bila hiyana akaniwekea gari tayari pamoja na vijisenti vya kuwapa wazazi na kuwa ningekaa kule kwa muda wa wiki mbili.

Kwa bahati mbaya sikuweza kukaa siku zote kwani kuna tatizo lilijitokeza ikanibidi nirudi mapema bila kumwambia nikijua tungejadiliana kunako nyumbani nikifika

Sikuamini kwani kufika nyumbani tena kwenye chumba.chetu cha kulala nikaona boxer ngeni nikamuuliza hii ni ya nani? Nakumbuka akanijibu kuwa ni ya shamba boy, nikajaribu kuuliza ilifikaje ndani kwetu akadai usiku alikuwa anaogopa hivyo akawa akilala na shamba boy.

Ulikuwa ni mtihani kwangu ingawa ilinibidi niamini huku nikijiuliza kama baba anakuwa muoga sie wana famialia tunaohitaji ulinzi wake itakuwa vipi? Basi yakaisha na maisha yakaendelea.

Ilipita miezi na sasa ni miaka ambapo wiki iliyopita nimemfumania live akiwa na jibaba la kiarabu tena bila aibu juu ya kitanda chetu cha ndoa.

Nilishtuka na kidogo nizirai lakini nilijikaza hasa ukizingatia sikutaka majirani wapate hili, kwa aibu akanifuata na kuniambia nimsamehe kwani ni mara ya kwanza na amefanya hivyo ili apate deal la kwenda Dubai kufanya shoping ya nyumba na ofisi yetu mpya.

Kweli niliamua kumuachia nyumba na nimeondoka na wanangu mpaka sasa nipo nimepanga sehemu ambapo nimeanza maisha mapya na kamwe hata niona maana ni laana.

Nawaasa vijana wasiwe na  haraka ya kukimbilia maisha mazuri, one step at a time.....

Dunia imeisha

MAPENZI: Linex amwagana na DEMU wake wa Kizungu...kisa ni Pesa na Muziki.


Kilichokua kinafata ni ndoa ambayo ilikua imepangwa na wote wawili baada ya Linex kukamilisha hatua muhimu ambayo ni kumvisha pete mchumba wake anaitwa Suvi raia wa Finland mwezi March 2013.
 

Millardayo amepata nafasi ya kuzungumza na Linex 
kwenye exclusive interview ambayo amekiri ni kweli imebidi kila mmoja aendelee na maisha yake na mapenzi yao kuisha kwa sababu kadhaa zilizojitokeza.
 
Sababu kubwa ni Suvi kutaka Linex ahamie Finland moja kwa moja na kwenda kuanza maisha mengine kwenye hiyo nchi ambayo ndio ingekua mara yake ya kwanza kufika, namkariri Linex akisema ‘kwa nia nzuri kabisa imekua ngumu kwangu kukubali hayo maamuzi, nataka kuendelea kufanya muziki wangu nyumbani’
‘Tayari nimetumia miaka zaidi ya 10 kutengeneza jina langu kwenye muziki hapa Tanzania, bongo mimi naishi vizuri na familia yangu naisaidia… sina tatizo la kuhangaikia maisha kwa kiasi hicho cha kwenda kuanza tena, yani ni sawa na mtu ameshaanza chuo mwaka wa kwanza alafu mtu anataka kukurudisha darasa la kwanza’
 
Sababu nyingine ni ‘mimi nimekua upande sana wa mama yangu, tayari nimeshanunua kiwanja namjengea mama yangu na biashara pia hivyo siwezi kuacha hii mipango isimame kwa sababu ya mapenzi, siwezi kuondoka kwenye maisha yangu kwenda kwenye maisha mengine sababu ya mapenzi’
 
Linex na Suvi walikua wamepanga kuoana lakini kwanza ilikua Linex anatakiwa kwenda Finland kutambulishwa manake ndugu wa mke mtarajiwa walikua wanamsikia tu hawajawahi kumuona, kisha angekwenda Finland kufunga ndoa alafu arudi tena Tanzania kufanya sherehe kisha aondoke moja kwa moja kuhamia Finland’
 
Ndoa ilikua inatakiwa kufungwa kabla ya february 2014 ambapo uhusiano wao umedumu kwa miaka miwili… baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwenye ndege Linex akitokea Nairobi ambapo Suvi  alikua anatokea Finland na kuja Tanzania/Afrika kwa mara ya kwanza, Linex akamfanyia ukarimu ikiwa ni pamoja na kumpeleka mpaka hotelini’
 
Kwa kuwa Suvi hakuwa na simu kwa wakati huo, Linex alimwachia namba ya simu lakini Suvi alikua kimya kwa kipindi chote cha mwezi mmoja mpaka siku moja Linex alipokutana nae Mlimani City Dar es salaam ndio urafiki ukaanza, Linex akawa anamtembelea hotelini na Suvi akawa anakwenda nyumbani kwa Linex kwa kipindi cha miezi minne ndio wakaingia mapenzini.

Credit: MillardAyo 

Video ya wabunge wa Upinzani wakitoka NJE ya Bunge baada ya Freeman Mbowe kutimuliwa leo mchana.



Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Mbowe alitolewa nje ya Bunge leo  mchana baada ya kukaidi amri ya Naibu spika Mh Ndugai alipomwamuru akae na Mh Mbowe kutokutii amri hiyo. 

Mh ngudai aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje, hata hivyo baadaye wabunge karibu wote wa upinzani walitoka pia isipokuwa Mh. Augustin Mrema wa TLP. 

TAZAMA  VIDEO  YA  TUKIO  ZIMA  HAPO  CHINI.


Mwanafunzi wa darasa la pili huko PWANI abakwa na wanafunzi wenzake wanne na kuharibiwa vibaya




MATUKIO ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa. 


Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao. 
"Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.
 
Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.
 
"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu," alisema Lwiza.
 
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.
 
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
 
"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.
 
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.


-Majira

SULUHU YA MGOGORO KATI YA DAYNA NA DIAMOND KUHUSU my number 1 HII HAPA


Baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy  ameamua  kukata  mzizi  wa  fitina  kwa  kuuanika  ukweli  wa  mambo....

Akiongea  na  #Team tizniz,Shedy  amefunguka  kama  ifuatavyo: 

“Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu.


"Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo  niliyonayo.

"Bila  hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali  kama  mteja,  ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo.
 

"Baada  ya Diamond   kuupenda  mdundo  huo, niliamua  kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,

"Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali  yeye  mwenyewe."

Tuesday, September 3, 2013

HAWA NDIO MABILIONEA 10 WANAO ITIKISA TANZANIA.............

KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Dk. Reginald Mengi.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana…
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Dk. Reginald Mengi.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
Said Salim Awadh Bakhresa.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9.  YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.



10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka.

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO


Siri  ya  Aunt Ezekiel  kupigwa  chupa  club  na  kujeruhiwa  mkono wake imefichuka.Habari  za  uhakika  zinadai  kwamba  Aunt  alipigwa  chumba  na  mrembo  wa  kike  katika  harakati  za  kugombea  penzi  la  mwanaume...

 Mwanaume  aliyekuwa  akigombaniwa  ni  Jeff  ambaye  anadaiwa  kuwa  ni boyfriend  wa  Yvonne ( aliyempiga  aunt  chupa )..

Kutokana  na  aibu  hiyo, mastaa  kadhaa  wameongea  na  mpekuzi  kwa  nyakati  tofauti  na  kueleza  masikitiko  yao  dhidi  ya  aunt  Ezekiel  ambaye  ni  mke  wa  mtu... 

Katika  maongezi  hayo, mastaa  hao  walidai  kwamba  mambo  anayofanya  aunt  hayaendani  na  matendo  ya  mke  wa  mtu. Aunt amekuwa  ni mtu wa baa, club  na  madanguro  mengine  ya  usiku, hali  inayotia  shaka  uhai  wa  ndoa  yake. 

" Aunt  kapata mume mwelewa sana  ambaye  kakiheshimu sana  kipaji  chake  kwa  kuto-mbana.

"Cha  ajabu yeye ameanza  kufanya  mambo ya aibu  kwa kuendekeza ngono  nje  ya  ndoa  yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..

Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa  tayari  kuchorwa  mtandaoni  alisema:
  
 "Aunt ajiangalie sana.Yeye  ni mke wa mtu kwa  sasa. Kitendo  alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini  atampoteza mume wake... 

"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi  siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"

sakata la madawa ya kulevya bado bichi sasa ni DIAMONDI & MASANJA MKANDAMIZAJI


Ni mwendelezo wa Sakata la unga ambalo sasa ni janga kwa taifa letu. Orodha zinaendelea kutoka na kuwekwa wazi huku bunge likivutana kuhusu sakata hlo.

Tetesi za kutoka ndani zinasema msanii wa muziki Naseeb Abdul au Diamond ambaye alijitapa wazi mbele ya kamera za habari kuwa anamiliki ukwasi zaidi ya bilioni moja kwenye akaunti yake, nyumba 5 za thamani Kijitonyama na Mikocheni na anatumia simu 6 za thamani ambazo zipo hewani muda wote tayari amenyang'anywa hati yake ya kusafiria na baadhi ya simu zake katika mwendelezo wa uchunguzi juu yake unaofanywa na vyombo vya dola.

Msanii pia wa maigizo Masanja Mkandamizaji ambaye anadaiwa kumiliki mkwanja mrefu na nyumba za thamani kubwa mpaka magari naye tayari ametajwa kuhusika na sembe.

Episode inaendelea,tuungane katka vita hii.

SOURCE: JF

Sunday, September 1, 2013

DIAMOND ATUHUMIWA KUIBA WIMBO WA DYNA..."MY NUMBER ONE"

 Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha,Msanii Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma nzito  baada ya  madai   kwamba wimbo anaotaka kuuachia wa No.1ni wa Dayna.

Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote.


Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna. Hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia. 


Sikiliza demo  hiyo  hapo chini.

BADILIKENI:PICHA ZA UCHI ZA PENDO ZAANIKWA BAADA YA KUSHINDWA KULIPA DENI


Picha  za  uchi  za  mrembo  Pendo  zimeanikwa  hadharani  na  mmiliki  wa  club  maarufu  ya  Westland  baada  ya  binti  huyo  kushindwa  kulipa  deni  lake.....

Taarifa  zinadai  kwamba  Pendo  alikopa  pesa  toka  kwa  mmiliki  wa  club  hiyo  na  kuahidi  kuirejesha  pesa  hiyo  siku  ya  alhamisi  iliyopita....

Wakati  wa  mkopo  huo, Pendo  alipigwa  picha  za  uchi  kama  dhamana  na  akaahidi  kwamba  endapo  atashindwa  kurudisha  pesa  hiyo, basi  picha  zake  zianikwe  hadharani...

Siku  ya  mkataba  ilifika  huku  Pendo  akiwa  hana  hiyo  pesa.Hali  hiyo  ilimfanya  jamaa  azianike  picha  zake  kama walivyokubaliana.

Saturday, August 31, 2013

Sumu ya nyuki inavyoangamiza VVU

USIFANYE HIVI NI PICHA TU

Wengi tunafuga nyuki, tunakula asali lakini hatujui kama nyuki wana faida zaidi ya hizi hapa.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi.

DIAMOND ONCE AGAIN:DIAMOND NA LINAH WANASWA WAKITOMASANA HADHARANI


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
  

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
 

Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.


Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
  
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.

AIBU NYINGINE:::::IGP aibiwa upanga wa dhahabu



Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.

SOMA ZAIDI

Thursday, August 29, 2013

TEAM TRUTH 18+:::: JINSI YA KUFIKA KILLENI MAPEMA KWA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA.


Kama ambavyo wengi tunatambua kuwa sehemu kubwa (asilimia 99.5) ya kufurahia ngono ni Mapenzi ya kweli juu ya mpenzi wako ikisaidiwa na utundu wako wewe mwenyewe manamke na sio mwanaume japokuwa baadhi ya wanawake hutegemea wanaume wawafanyie kila kitu mpaka kuwafikishe.

Wakati mwingine wanaume huchoka kwa vile kwa kawaida wanawake tunachukua muda mrefu zaidi kufikia mshindo ukilinganisha na wanaume, kwamba mwanamke anafika ndani ya dakika 10-15 wakati mwanaume anafika ndani ya dakika 1-5 unless awe anajua kujizuia nahapo ndio atakwenda mpaka dakika 45 na baadhi huondoka zaidi ya hapo kutokana na kutosisimuliwa vilivyo (yaani akikupanda hamalizi mpaka uke unakauka na wewe hamu inakuishia) hahahahaha!


Well, back to topic......


Mbinu ya kuita kilele sio ngumu kama wengi mlivyokuwa mkifikiria/dhania bali ni ya kawaida sana na utashangaa ni jinsi gani inafanya kazi, na ikiwa umebahatika kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kujizuia basi unaweza kupiga 3 ktk mzunguuko wa kwanza.


Unapokuwa ukifanya mapenzi hakikisha akili yako yote iko kwenye kufanya mapenzi, sio lazima umfikirie mpenzi wako bali unaweza kufikiria chochote kitakacho kufanya "unyegetuke" zaidi wakati "mzigo" uko ndani ya uke sio.


Mfano unaweza kuwaza/kujisemea "nat......... sasa", unaweza kumuuliza mpenzi wako akuambie anafanya nini in rude way (it works 4 me), au kama anakujua vizuri basi anaweza akaanza kusifia Uke wako ulivyo, anavopenda kukufanya n.k (wengine nasikia huomba kutukaniwa wazazi wao.....hey it works 4 them so jaribu na wewe)


Jinsi jamaa anavyokufanya wewe pia msaidie.......well jisaidie na hakikisha unahangaika kupata "kipele" (mahali unaposikia raha zaidi pakiguswa), ukisha hisi mwambie atulie hapo hapo na wewe anza kufanya "makaratee" zunguusha kiuno chako ktk pembe zote (badilisha mirindimo) na wakati unafanya hivyo hakikisha unabana pumzi na kuiachia papo kwa hapo (hakikisha huiachii kwa muda mrefu yani in sec unabana na kuiachia).


Psssssssssssi: Sometimes u have 2 be a little selfish ei? Wanaume wakibana pumzi wanachelewa kufika lakini mwanamke ukibana pumzi unawahi kufika.....hii ni kutokana na uzoefu na nime-share na baadhi ya wanawake na wamefanikiwa kufurahia ngono kama ninavyofurahia mimi.


Karibu sana na kila la kheri ktk jaribio hili

Team Truth (Dinahicious)::::Ni kweli Wanaume wanapenda "Saa sita" Kifuani?


Sina hakika ni kwanini wenzetu (wanaume) wanapenda Matiti wakati sisi (wanauwake) ndio tunao....... ikiwa yatafanyiwa "kazi" vizuri na kwa utaalam. Ukiachilia mbali hilo, matiti hutufanya tuhisi kuwa ni "wanawake" pia ni Mwanzo mzuri wa maisha ya mtoto).


Nakumbuka mara ya kwanza kuvaa Sidiria ilikuwa 2003, sikuwa nahitaji lakini nilidhani kuwa kuvaa Sidilia ndio "uanamke", basi nikaenda kupima size ya Matiti ili kupata "Bra" itakayonitosha vema. Wahudumu wakanishangaa na kusema kuwa ninge-save pesa nyingi kwa kutovaa "Bra" kwani sihitaji, lakini kwa vile nilitaka kujihisi kuwa ni mwanamke nilisisitiza kupata "Bra" yangu ya kwanza....TMI i know, sorry hihihihi....


Katika hali halisi hakuna Mwanaume anaependa kukutana na mwanamke ambae matiti tayari yapo tumboni (inategemea na ukubwa), hiyo haimfanyi mwanaume huyo kuchukia matiti yaliyoanguka ila angependa yaanguke akiwa Mkewe na sababu  iwe ni kunyonyesha watoto wao.


Hebu badilishakibao wewe ndio uwe mwanaume etii....alafu unakutana na na titi zipo tumboni, hapo hajanyonyesha/Zaa, utakuwa hujui raha ya  matiti yaliyosimama na pengine siku moja ungependa kupata uzoefu huo....Hebu fikiri.


Kwa bahati mbaya wanawake wengi kwenye jamii rejea topic ya Jinsi ya kutunza, wengi hujiachia tu kipindi ambacho matiti hayo yanahitaji "support". Hakika Matiti kuanguka ni kutokana na kunyonyesha watoto wa Mumeo, lakini kumbuka kuwa sio Wanawake wote wenye matiti yaliyoanguka wamenyonyesha, Wamezaa, Wametoa mimba au wanawaume/wapenzi....kwamba matiti yao yalianguka kitambo kabla hawajanyonyesha kutokana na kutoyatunza vema.


Ikiwa mumeo alikukuta ukiwa na matiti Saa sita bila shaka ataendelea kuyapenda akijua kuwa wanae waliyatumia "early days of their lives", obviously atakuwa amekubali mabadiliko uyapatayo kutokana na Uzazi....lakini at least aliyakuta Wima na yeye ndio kachangia yatazame Chini (baada ya kunyonyesha watoto).


Ukweli wenye maumivu ni kuwa, Asilimia kubwa ya wanaume wangependa matiti ya wake zao au wapenzi wao yadondoke wakiwa nao na sio wayakute yakiwa hivyo (matiti yamedondoka). Hali inayofanya wengi wao kuzungumzia u-wima wa matiti na kucheka au kubatiza yale yaliyolala kuwa ni Malapa.


Mimi binafsi huwa sipendezwi na hilo na siku zote huwa nasema kabla hujamcheka mwanamke mwenye matiti yaliyolala hakikisha wanawake kwenye familia yako bado matiti yao yapo wima na muhimu kabisa ni je Matiti ya mama yako uliyonyonya bado yamesimama(saa sita)?


Ikiwa kwa bahati mbaya wewe ulichelewa ama ulikuwa hujui namna ya kutunza matiti wakati yananza kujitokeza hakikisha Wanao wa kike wanajua(wafundishe), pia hakikisha unayapa "support" yakutosha unapofanya Mazoezi, Unapo karibia hedhi, unapokuwa Hedhini, utakapo kuwa Mjamzito na wakati unanyonyesha.

CHUPI NA SHANGA ZA MSANII SHILOLE ZAANIKWA NJE- FIESTA



 

UPDATE: MAJAMBAZI YALIYOVAA SARE ZA POLISI YAVAMIA HABIB AFRIICAN BANK NA KUPORA MAMILIONI




Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha.


 Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo..

Habari  zaidi  baadae. 

TRAFFIKI FEKI ALIYEKAMATWA HIVI KARIBUNI ALIKUWA NI MFUNGWA WALIYETOROKA GEREZANI




MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani.

Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.

Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.

“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.

“Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.

“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.

“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.

Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.

Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.

Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:

“Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”

Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.